Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,664
- 47,058
Shetani ameingia kwenye nchi yetu, anayetaka kutuaminisha kuwa uhai wa mwanadamu si chochote, unaweza ukauondoa wakati wowote unaoutaka, tena kwa sababu za kipuuzi kabisa, eti wanakosoa Serikali.
Vyeo na madaraka hupewa mtu yeyote ambaye wanadamu wameamua, lakini tujue kuwa hata katika umoja wetu unaojumuisha zaidi ya watu milioni 60, hatuna uwezo wa kuurudisha uhai wa hata kiumbe kimoja kilichopotezwa.
Nchi hii ina watu wengi wenye uwezo wa kuwa Marais lakini hatuna hata mmoja mwenye uwezo wa kurudisha uhai wa hata binadamu mmoja ambaye uhai wake umepotezwa na wauaji waliopo ndani ya vyombo vya usalama.
Tulikuwa na Rais, Baba yetu wa Taifa Mwalimu Nyerere, aliondoka, tukampata Mwinyi; aliondoka, tukampata Mkapa; aliondoka, tukampata Kikwete; aliondoka, tukampata Magufuli; aliondoka, na sasa tuna Samia. Hii inatuonesha kuwa hakuna wakati nchi itakosa watu wa kuwa Marais. Kuondoka kwa Rais mmoja, tunazo replacements nyingi za kuendelea kuongoza nchi.
LAKINI hao Marais wote waliopita, na hata wa mataifa mengine, na watakaokuja, hakuna hata Rais mmoja, mwenye uwezo wa kurudisha uhai wa waliouawa na wasiojulikana tunaowajua. Ukweli huu, ndio unaotoa uthibitisho kuwa Urais, Umakamu wa Rais Uwaziri Mkuu, si chochote, si lolote mbele ya uhai wa mwanadamu. Kwa kuwa Rais hana uwezo wa kurudisha uhai wa mtu ambaye uhai wake umepotezwa na watekaji na wauaji waliopo ndani ya vyombo vya dola, hivyo kila kiongozi anatakiwa atumie uwezo wake wote, kuhakikisha uhai wa wananchi anaowaongoza hauondolewi hovyo hovyo kama inavyotokea sasa, tena ukifanywa na vyombo vya Serikali viliyotakiwa kuwalinda.
Kiuhalisia, Serikali au Rais aliyeshindwa kutekeleza jukumu hili kuu la msingi, anakuwa ameshindwa uongozi, na kama ni muungwana, anatakiwa kuachia nafasi ili apatikane mwingine alibebe jukumu hilo la usalama wa watu kwa nguvu zake zote.
Tuna shida ya kushindwa kuurudisha uhai wa mwanadamu, hatuna shida ya kumpata Rais mwingine, ikiwa aliyepo akaondoka kwa sababu zozote zile, kama kushindwa kutimiza jukumu lake la msingi la kuwalinda raia.
Wananchi tusiwe na hofu ya mabadiliko ya uongozi 2925, tuwe na hofu ya sisi wenyewe na ndugu zetu kutekwa na kuuawa.
Na Rais Samia, kwa vile inaonekana hili suala la kuwahakikishia ulinzi na usalama wananchi, inaonekana ni mzigo mzito kwake, asione shida, kuamua kutogombea mwaka 2025 ili nchi impate mtu mwingine. Hakuna mwanadamu anayeweza yote. Rais Samia kuna aliyoyaweza, tunamshukuru kwa hayo, lakini hili amelishindwa. Na bahati mbaya amelishindwa lililo jukumu la msingi kwa kiongozi wa nchi.