nionavyo Mimi watanzania tupo vifungoni kama tujuavyo kwa wafungwa mwenye mamlaka ya kumuendesha mfungwa hakuna zaidi ya bwanajela. hivyo hivyo sisi tupo kama wafungwa ambapo viongozi na matajiri ndio mabwana jela wetu.
Si kitu kigeni Leo tajiri kuwahamisha watu pasipo kufata Sheria..si kitu kigeni viongozi wenye madaraka makubwa Leo kujimilikisha ardh zaidi ya heka 100 Mungu alitupa watanzania hadhina kubwa kuliko nchi yoyote duniani...tuna migodi Mikubwa mikubwa, mbuga zaidi ya tano kubwa, milima mikubwa maziwa kila kona, bandari, gesi nk.
Hivi vyote tusinge vitumia mpaka tupate elimu hayo yangekuja kunufaisha wajukuu zetu..lakini kutokana na ufinyu wa maarifa wa viongozi wetu na kujifanya wao NI wagunduzi wanaamua kugawa rasilimari zetu huku na huko wageni wananufaika...Ila tukae tufikirie miaka 50 wajukuu zetu watarisi nini? Mimi nawewe Leo tunawachekea viongozi wabovu ambao wanatusababishia laana kwa makusudi kabisa.
Ingekuwa ni mamlaka yangu ningesimamisha uchimbaji wa madini na uvunaji wa gesi kwasababu hatuna ujuzi wa kutosha juu ya matumizi ya vitu hivyo...