Watanzania ni watu wa ajabu sana.Wanapenda mabadiliko Lakini hawataki kubadilika.Wamekuwa na sifa ya kulalamika tu pasi kujuwa tatizo la malalamiko yao
Mtakumbuka utawala wa Nyerere mwishoni kabisa tulimchoka.
Akaja mzee Mwinyi ndo usiseme. Kaingia Mkapa pia pale mwishoni tulilalamika sana.
Kachukua Kikwete naye hivyo hivyo mwanzo tulimsifu sasa hivi malalamiko chungu nzima.
UKAWA wamekuwa wakisema mara zote,Tatizo sio mtu ni mfumo,Na bila kuuvunja mfumo huo.Tutaendelea kulalamika siku zote huku tukidanganywa tupo kwenye mabadiliko.
Sasa tunae Magufuli,Sintoshangaa ifikapo 2019 yakajirudia yale yale ya kulalamika"Tukisahau sifa tunazomwagia sasa"Tena tunalalamika na siku ya kura tunarejesha mfumo ule ule wa kiCcm tukitarajia mabadiliko.
Sasa najiuliza huu ni Ugonjwa?Na kama ni ugonjwa wa watz ipi dawa sahihi ya gonjwa hili"Gonjwa la Kulalamika"