Watanzania mjifunze kuheshimu watu wa aina yetu. Nimemwadhibu huyu bwana mdogo

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,189
6,441
Heri ya mwaka mpya. Nipo Dar siku 3 sasa nimetingwa kidogo majukumu ya ofisi n.k ila nashukuru nlipokelewa vizuri na member mmoja wa JF weekend hii tulikuwa wote tunakula Pizza pale Pizza Hut Mkuki na tukaangalia Cinema pamoja.

Nimetoka Airport muda huu kuna rafiki yangu nlitoka naye Sweden amekuja Tanzania a spend two weeks so leo alikuwa na safari ya ndani ya nchi kuna sehemu katangulia then weekend nitamfuata.

Wakati narudi nawahi ofisini nikamalizie kazi fulani then saa saba niwahi kupata lunch Serena Hotel kisha saa tisa nihudhurie meeting. Lililotokea jambo la kusikitisha kidogo kwangu.

Nlikuwa na Range Rover. Hii gari speed yake ni 280. Huwa nasikitika tu kuwa nakosa barabara za angalau kufikisha 180, maana kwa hizi barabara zetu unajikuta unaendesha gari speed ya mwendo wa kobe 100 au ukipata dakika chache kasehemu kafupi 120.

Basi kilichonikwaza mimi nimetoka airport nimevuka mataa fulani kabla ya daraja. Mimi nipo kwenye gari naona jamaa mmoja anakuja kasi na Toyota yake RAV 4. nikakaza mwendo naye eti akakaza mwendo. Niliona amenikosea heshima sana. Anataka shindana na Gari? tena RR?

Basi nikabongeza tu pedal ya mafuta kiasi gari ikachuchumaa kidogo, hizi gari unapoongeza speed inakumbatia ardhi au inachutama. Gari yangu ilichanganya mwendo haraka na jamaa nikahisi yeye alisimama ghafla maana nlimwacha kwa kasi ambayo kumbe maskini nilimtesa sana.

Yeye nadhani alikanyaga mafuta akili yake ikawa inataka ila Toyota Rav 4 inakataa. Sikumwona tena maskini, sielewi nini kilimpata nachosikitika ni yeye kukosa heshima kutaka kuover take gari akiwa na Toyota Rav 4.

Alinikosea sana hilo jambo lilinikwaza nikajiuliza hivi kwa nini watanzania tunakosa kuheshimiana? Hili jambo huwa nashangaa kabisa parking napark BMW au RR halafu anakuja mtu anapark Carina, Rav 4 ,vitz au sijui nini pembeni yangu.

Kibaya anapofungua mlango wa usafiri wake unagusa gari langu.hili jambo huwa sidhani kama ni sahihi.sipendi kabisa gari liwe linagusana na vifaa vingine vya usafiri.mwaka jana nliuza Ford Range kwa sababu kadhaa mojawapo ikiwa ni suala hilo la kuchunwa ubavuni.

Napenda gari ibaki na rangi yake ile ile toka Ulaya au Marekani.tujifunze kuheshiana mbona ni jambo la kawaida tu.mfano mimi nina gari siwezi enda park zinapopark ndege au boat binafsi.siwezi fanya hivyo ni kukosa nidhamu.

Kwa hiyo mwaka 2020 tujipange ndugu zanguni huu ndo muda wa kuanza mashambulizi tusisubiri dk za mwishoni.ukifunga mabao kadhaa then unabaki kulinda ushindi na kucheza mpira kwa ku relax. Haya maisha jitajidi uwe na viwango.acheni tabia ya kulinganisha kila kitu.

Kuna vitu haviwezi fanana hata iweje.anayeendesha Benz, Bmw, Range,J EEP, GMC hawezi fanana na anayeendesha Toyota, Nissan, Subaru n.k

Hata ukiwatizama hawa watu ngozi zao zipo tofauti, wanavyotembea hata kuongea ni tofauti sana. Mimi sehemu nyingi naenda nimevaa casual tu lakini naona wanavyoniheshimu. Siku moja nimekaa mgahawa mmoja wa hali ya chini pale posta siju ni Brake/ Break Point. Akashangaa kuniona pale. Nikamuuliza why akanambia mwonekano wangu ni kama nimetoka USA siku hiyo.

Nlimwambia naishi Sinza na sometime Kijitonyama akakataa kabisa kuwa hayo maeneo ya watu wa kipato cha chini siwezi kuwa na rangi hii.

Anyway ni maisha tu usikasirike. Mimi zamani nilipokuwa namchukia Mayweather akitumia pesa vibaya siku nalalamika mzee alishangaa sana. Akaniuliza kwa ukali whats wrong with you? Hizo si ni pesa zake? Katafuta kwa jasho lake? Why umpangie matumizi?

Mzee amekuwa akisema "son, tafuta pesa tu maisha wala si magumu kama watu wanavyosema. Maisha ni jinsi unavyotaka wewe yawe. Usimchukie mwenye pesa, usimchukie anayezungumzia maisha mazuri.
 
Endapo maneno mengi ila Kuna cha kujifunza raia tutafute hela si kung'aka tu huko mara huyu kafanya vile huyu hivi.. jengine la kujifunza ni la kuheshimu mahali si palipo na ndege unapaki gari😂😂
 
Na bado hawa wanawake waliojariwa sura bila akili wataamini hizi stori na utawagonga....dah
 
images (50).jpeg

Life behind the keyboard
 
Back
Top Bottom