Tanzania kuna redio nyingi sana amabazo 90% zina vipindi vya michezo mfano E fm, Wasafi, Resio one, Redio saut,kiss fm nk.
Kama wewe ni mpnz wa michezo utakubaliana na mimi kuwa kwa siku unaweza sikiliza zaidi ya vipindi viwil katika vituo vya redio tofauti.
Bnafsi huwa nasikiliza sana vipindi vya jion, katika vituo tofauti.
Redio nyingi kupitia vipindi vyao vya michezo kuna waongoza vipindi yaani watangazaji na pembeni yao wachambuzi wa michezo mfano, Eddo, Oscar Oscar, Mwl Kashasha, Edga Kibwana na wengineo.
Kuna kero mbili kubwa zinaboa,zinachefua na zinakeleketa sanaaaa ambazo hufanywa na baadhi ya wachambuzi na watangazaji wa vipindi hivo wa kike kwa wakiume.
KERO NO 1.
Kushindwa kutamka kwa usahihi majina ya wachezaji na timu hasa za inje.
Kwa mfano baadhi tu ya majina yanayowatesa kutamka ni >>>>>>borussia mönchengladbach
>>>>>>Eintracht frankfurt
Hayo majina ya hizo timu hapo yaan ni shidaaaa, unajiuliza mchambuzi wa michezo au mtangazaji unashindwa kutamka ,mkononi una smartphone za nini? ,goggle inafanyabkazi gani??.
Wakati unaandaa kipindi why usipitie majina unayojua yanakupa ahidaa.
Namsifu sana mchambuzi wa E fm anayeitwa maetral aka Kiungo mkongwe mpak huwa anawakosoa wanzake hadharani. Big up bra.
KERO NO 2.
Matumizi ya maneno ya kiswahi yasiyo na wingi kuyalazimishia wingi mfano .....
Usajiri wanatamka sajiri wakimaanisha wingi.
Ujumbe wanatamka jumbe wakimaanisha wingi.
Mnakeraaa sanaa .mnaboa sanaaa.halafu ni vijana ambao mnajiita wasomi wa vyuo vikuuu.
Kuna mchambuzi wa clouds fm kipindi cha saa tatu usiku michezo anapenda sana kuyatumia...Unaboa bra, kuna watangazaji na wachambuzi kiss fm na rwdio saut yaan kichefu chefu kweny haya maneno na wwngine wengi,
Tunawapongeza wachache mnaozingatia matumiz sahihi ya lugha ya kiswahili na kingereza katika matamshi ya majina.
Wewe nani anakukera katika haya.