Watangazaji wa Kipindi kinachozidi kujizolea umaarufu nchini cha DADAZ cha EATV wana Waume wangapi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Kwanza nianze kwa Kuupongea Uongozi wa EATV kwa kuja na Kipindi kama hiki ambacho ni kizuri sana na pia nichukue nafasi hii kuwapongeza sana Watangazi wake kuanzia kwa Program Brand Manager wake Scola Kisanga akiwa na Wenzake akina Dellaida na Mwanne Othman bila kuwasahau na Mtangazi mwenzao mmoja aitwae Paulina kwani wanakitendea haki Kipindi na labda kabla sijaenda mbali nami GENTAMYCINE niseme au niweke wazi kuwa ni mmoja Watazamaji wao mkubwa sana nikipata muda kila asubuhi ya Saa 5 hadi Saa 6 kila Jumatatu hadi Ijumaa na kama nikikosa huo muda basi huwa natizama marudio yao kila Saa 2 hadi Saa 3 usiku Jumatatu hadi Ijumaa.

Baada ya ' Kuwasifieni ' sasa nawaombeni mnivumilie kidogo ili niwapeni ' Sindano / Dozi ' japo najua kama hamtokasirika na mkiyafanyia Kazi haya mawazo yangu machache basi Kipindi chenu kinaweza sasa kikawa bora zaidi ya kile cha SHILAWADU ambacho Mimi na ' Kichaa ' mwenzangu tunakitizama sana kila Ijumaa Saa 3 hadi Saa 6 usiku.

Sina shida na ' Segments ' zenu Nne ambazo zimekaa vizuri sana Kimpangilio na ndiyo maana zimeweza hata Kunivutia na Mimi GENTAMYCINE nikawa ni Mtazamaji wenu mtiifu na wa Kutukuka kabisa.

Kero yangu hasa ipo kwa Watangazaji ambao wao kila Siku wakiwa katika Kipindi Kazi yao ni kupeana tu Historia ya Mabwana zao na Idadi ya Wanaume waliowahi kuwa nao kana kwamba Sisi Watazamaji wao wote tuko pale kujua idadi ya Wanaume waliolala nao wakati wamesahau kwamba hata Sisi wengine huku tumeshakuwa na Mahusiano na Wanawake ambao ukiwapanga Dar hadi Kigoma wanaenea ila ' tumeuchuna ' tu na Siri zetu mioyoni.

Mtangazaji # 1 Scola Kisanga

Uko vizuri sana na Kipindi chako unakitendea haki ila punguza sana ' Kutunga ' idadi ya Wanaume uliowahi kuwa nao. Halafu punguza sana Kukatakata Viuno hovyo ukiwa unatangaza. Najua unaweka vituko vyako hivyo ili labda uzidi kuteka Watu ila kumbuka kwamba huangaliwi tu na Wanawake wenzako wa mjini bali wapo pia hata Mama zako na Mabinti ambao na wao pengine wangetaka Kujifunza kitu Kwako.

Pia punguza sana kujisahau ukiwa unazungumza hadi unatoa Siri zako na madhaifu yako ambayo kwa Mwanamke kama Wewe sidhani kama yatakusaidia sana na pengine unakaribisha ' Maadui ' wa ama Mahusiano au Ndoa yako kama umeshaolewa. Maneno kama sijui unapenda Hela sana au Mwanaume akitaka akuteke zaidi basi awe anakuletea Chupi tu Nyeupe sidhani kama yana tija sana. Halafu punguza sana kuchekacheka hovyo utadhani Bata Mzinga anataka kwenda Bwawani Kuogelea.

Mtangazaji # 2 Dellaida

Hata Wewe pia uko vizuri sana japo kuna muda huwa unaharibu kwa kupenda sana kuzungumza Kiingereza utadhani uko Uingereza ambako naambiwa umeshawahi kuishi ( kama sijadanganywa manake Watanzania kwa Kudanganyana tu hatujambo ) ila jua kwamba uko nchini Tanzania ambako Watazamaji wenu 75% wanazungumza Kiswahili.

Udhaifu mkubwa ulionao Dellaida ni Kucheza na Camera na unapenda sana Kututumbulia ' mimacho ' yako mikubwa utadhani Refarii Mstaafu Collina ameona ' Faulo ' imetokea Uwanjani. Hebu jaribu sana kufanyia Kazi zoezi la kutokupenda kuiangalia sana Camera pindi ukiwa katika Kipindi chenu hicho kwani itatufanya tuhisi labda ' You're not a Professional ' katika Television Broadcasting.

Mtangazaji # 3 Mwanne Othman

Kama kuna Kitu ambacho nakipenda kwako ni ' Uchangamfu ' wako na jinsi unavyojua Kuutumia vizuri mwili wako Pipa / Simtank ( Mnene ) kwani kuna Wenzako wana huo huo Unene ulionao lakini wakikaa katika Kiti wakitaka kuamka lazima Kwanza waombe ' mwongozo ' kwa Spika ( namaanisha waombe msaada wa Kuamshwa ) ila Wewe uko ' Fiti ' mno.

Udhaifu wako mkubwa najua unapenda Kuimba sana na una Kipaji cha Kuimba pia ila kuna muda huwa unazidisha unakuwa unaimba hadi sasa unaboa na kupiga Kelele na nadhani itabidi siku zingine ukiwa unaimba basi Uongozi wa EATV uwaweke kabisa Wapiga Vyombo ili wakupa ' backup ' ya kutosha. Punguza kidogo.

Mtangazaji # 4 Paulina

Kama kuna Mtangazaji wenu ambaye anaongoza kwa mvuto na urembo pindi muwapo hapo Kipindini basi ni huyu Dada Paulina. Anavutia sana kumuangalia na ana Sauti ambayo inavutia sana na ya Kimahaba zaidi. Sijajua na sina uhakika kama nae mpo nae moja kwa moja au ni ' Mtangazaji Deiwaka ' ila kama bado hamjamuajiri nashauri muandalieni mkataba kwani ataongeza kitu / mvuto fulani katika hicho Kipindi.

Udhaifu wako mkubwa Paulina ni kwamba kuna muda huna ' Confidence ' halafu unajishtukia mno na kama vile unababaika. Kisha kuna namna fulani hivi ambavyo huo Mdomo wako huwa ' unaibinua ' kama vile ' Kiumbea ' fulani au unataka ' Kumshushua ' Mtu. Jaribu tu kuwa ' neutral ' na amini kuwa unaweza na usiogope.

USHAURI WANGU JUMUISHI

Naomba Uongozi, Waandaaji na Watangazaji wahusika wa Kipindi hiki cha DADAZ wafanyie Kazi hasa ' Segment ' ya Nne ambayo binafsi naiona kama vile ni ' irrelevant ' na badala yake jaribuni Kubuni kitu Kingine hapo ambacho kitaleta mvuto zaidi.

Na ikiwezekana zaidi kwakuwa Kipindi ni cha DADAZ basi nadhani hata 99.9% ya Wageni wenu wawe ni Wanawake wenzenu na siyo Wanaume kwani uwepo wao hapo Studioni kwa kiasi fulani kunapoteza ladha nzima ya Kipindi chenu.

Namalizia tena kwa kusema pongezi na hongereni sana EATV kwa kuja na Kipindi hiki cha DADAZ ambacho hata Mimi ambaye ni Mwanaume kuna Elimu kubwa naipata hapo na Maarifa mengi pia najifunza ambayo naamini yanaweza siku moja kuja kunisidia pale nikiamua rasmi sasa kuwa na Mwenza wangu ndani na Kuanzisha Familia kwani huwa kuna ' madini ' mengi nayapata.

Mwenyezi Mungu akibariki hiko Kipindi na awabariki Watangazi wote na mkae mkijua kwamba GENTAMYCINE nawakubali na nawapenda mno halafu ni Mtazamaji wenu mtiifu kabisa na nikikosa hicho Kipindi huwa nahisi nimekosa vitu vingi hasa vinavyohusu Mahusiano na Tabia za Kijamii kwa ujumla.

Mengiyo nawaachia Members wengine wa JamiiForums ambao nao pengine ni Watazamaji wenu waweze Kuchangia na Kushauri ili basi mwisho wa Siku Kipindi chenu kiwe kizuri zaidi ya kilivyo sasa. Mtanisamehe pia kama ' madongo ' yangu yatakuwa yamewakwazeni ila naamini nami nitakuwa nimesaidia Kitu fulani katika kuwawekeni sawa na kuwa vizuri zaidi Kiutendaji na Kiutangazaji.

Nawasilisha.
 
Hivi syo kinawahusu mabinti jamani au

Umeshaona wakuzuia Wanaume Kukiangalia? Na kama kinawahusu tu Wanawake / Mabinti hadi Wanaume tena wale ambao ni ' maarufu ' na ' muhimu ' katika Jamii yetu na kwa Kada mbalimbali huwa wanaalikwa? Hivi ni Kwanini Watanzania mnakuwa ' Wapumbavu ' hivi katika kufanya ' logical arguments ' kadri siku zinavyoenda mbele?
 
Umeshaona wakuzuia Wanaume Kukiangalia? Na kama kinawahusu tu Wanawake / Mabinti hadi Wanaume tena wale ambao ni ' maarufu ' na ' muhimu ' katika Jamii yetu na kwa Kada mbalimbali huwa wanaalikwa? Hivi ni Kwanini Watanzania mnakuwa ' Wapumbavu ' hivi katika kufanya ' logical arguments ' kadri siku zinavyoenda mbele?
Au siyo
 
Mkuu kila kipindi kinaendana na maudhui yake kwa mapendekezo yako ungesubiri tu kutizama taarifa ya habari ukalale,ndio maana wamekiweka kipindi kuanzia saa3

Ushauri una mambo mawili ama ukubaliwe au ukataliwe na hakuna mahala popote nimewalazimisha wafuate kile nilichosema. Jifunze Kusoma Uzi, Kuuelewa na Kuheshimu mawazo ya Mtu. Pumbavu!
 
Ushauri una mambo mawili ama ukubaliwe au ukataliwe na hakuna mahala popote nimewalazimisha wafuate kile nilichosema. Jifunze Kusoma Uzi, Kuuelewa na Kuheshimu mawazo ya Mtu. Pumbavu!
We jamaa ni boya sana
 
Jamaa thread zake ni magazeti, halafu pumba tupu.

Na kamwe usingejua kama ni Magazeti bila ya Wewe pia kuwa Msomaji wa hayo hayo Magazeti yangu. Na Uandishi wangu huu huu wa Kimagazeti ndiyo unafanywa niwe ' Followed ' na Watu zaidi ya 47 humu lakini pia ID yangu ikiwa ni miongoni mwa ID's ambazo zinaongozwa Kupitiwa na Kufuatiliwa kila siku. Na kama haitoshi ni Uandishi wangu huu huu wa Kimagazeti ndiyo unafanya niweze kuleta ' impact ' hasa yale maeneo ambayo huwa nayagusia katika Mada zangu mbalimbali. Na pia ni Uandishi wangu huu huu wa Kimagazeti ndiyo unafanya hadi Mitandao na Redio mbalimbali hapa nchini Kupenda kutumia ' Maandiko ' yangu ili kuwavutia zaidi ' walaji ' wao. Na mwisho kabisa ni Uandishi wangu huu huu wa Kimagazeti wa GENTAMYCINE ndiyo umepelekea hadi Taasisi muhimu na Ofisi ya anayekuongoza hapa Tanzania wawe ' wanaikodolea ' hii ID kila uchao ili kuona naandika nini na najivunia kuwa kati ya mambo ambayo huwa nayaandika hapa basi 75% yake huwa yanazingatiwa na kufanyiwa Kazi.

Chuki zenu Kwangu ndizo zinanifanya hadi muwavutie Watu wengine hapa kupenda kunifuatili hivyo nakuomba Wewe na ' Wapumbavu ' wenzio ambao mnachukizwa na kukerwa na hii ID msiache Kunichukia kwani ndiyo ' mnanipaisha ' zaidi hadi kuwa na mvuto wa Kipekee unaohitimishwa na ' Signature ' yangu isemayo ' Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer '.

Nasubiri sasa kusikia na Wewe ambaye huandiki ' Magazeti ' una ' impact ' gani katika uwepo wako hapa kama Member ili nami na wengine waweze Kuupima ' vividly '. Na hamtoweza Kunivunja moyo wala Kunirudisha nyuma kwa lolote na kama bado nipo Hai hivi nitaendelea kuwepo hapa Jamvini 24/7 na kuandika mambo mbalimbali, kufanya chambuzi zangu za Kiuandishi na za Kimawazo na kutoa maoni mbalimbali ya Kimaarifa katika yale ambayo nayajua na nayaamini.

Mwisho kabisa Utafiti mdogo ambao nimeshaufanya humu na kuna siku nilishasema na leo naurudia tena ni kwamba 95% ya wale Members wanaojifanya ' Kunichukia ' au ' Kukereka ' nami ' actually ' ndiyo Members ambao ' wananikubali ' na hawaachi kunifuatilia hapa kila Uchao kujua nimeandika nini na kuna wengine japo mkiwa hapa mnajifanya Kunichukia ila mawazo na maono yangu huwa mnayachukua na kuyatumia sana huko mlipo na kuonekana mpo vizuri wakati kumbe mmemchungulia ' Mwanamume ' humu.

Na siku zote Uandishi wangu hapa Jamvini ukiwa ' Mpumbavu ' kama ulivyo pamoja na hao Wenzako hutoweza Kuujua na Kuuelewa ila mwenyewe najua natumia mbinu gani na ipi ya Kiuandishi ili niweze Kufikisha ujumbe ' Kusudiwa ' na kuna muda huwa naweka ' Upuuzi ' fulani ambao ndani yake kuna Ujumbe na nashukuru Watu ' Werevu ' huwa wanakuwa wepesi kunielewa na tunaenda sawa. Najua ' Natural Charm ' yangu ndiyo inawasumbueni na kuwatesa ila nadhani kama ni wa kumpelekea hizo ' Chuki ' zenu basi mzielekeze kwa Mwenyezi Mungu aliyeniumba na ' Kunibariki ' hivi nilivyo na kuwaacheni nyie hivyo mlivyo.

Usisahau pia ' Kuwafowadia ' ujumbe huu adhimu kabisa ' Wapumbavu ' wenzio wote na wale wataojitokeza huko mbeleni.

Nimemaliza.
 
Back
Top Bottom