Watangazaji wa Clouds Media, Wampiga Stop Tundu Lissu kutaja jina la Abdul kwamba alimpelekea Rushwa. Idrissa Rubibi na Daniel Naftari wadakwa na Pesa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,689
55,662
Maelezo ya Tundu Lissu

*Mimi wanasema sina pesa. Na kama sina pesa sina pesa za kugawa.

*Mimi sitoi Rushwa na Sipokei Rushwa. Nililetewa hapa kwenye Sebule hii na Abdul

Mtangazaji: Mheshimiwa tunaomba tusitaje Majina.

Tundu Lissu: Kwanini nisitaje kama vinaweza vikathibitika?

Mtangazaji: Eleza tu maelezo. Sisi ni Chombo cha habari.

Tundu Lissu: Kama mnataka mambo mengine yafichwe hiyo ni juu yenu

Mtangazaji: Unaweza kusema lakini bila kutaja Majina

Tundu Lissu: Hapana, kwanini unaruhusu nitaje jina la mwenyenyiki nitaje jina la nani lakini hutaki nitaje jina la waovu hawa?

Mtangazaji: Endelea

Tundu Lissu: Mimi sitoi Rushwa sipokei Rushwa. Mimi ni msafi.

*Watu wanatembea na Mabegi ya pesa sio watu wangu. Sio watu wangu waliooneshwa wakigawa pesa Ubungo Plaza sio watu wangu

*Nimekemea Rushwa hadharani. Mgombea gani mwingine amefanya hivyo?

*Pesa zinatoka kwa wale wasioipenda chadema. Wale wanaotaka waichafue chadema.

*Waliokamatwa wakigawa pesa ni Kampeni Meneja wa Mwenyekiti Mbowe anaitwa Daniel Naftari. Yupo kwenye Video amefukuzwa Ubungo Plaza

*Aliyekamatwa anagawa pesa Chooni anaitwa Idrissa Rubibi mgombea wa nafasi ya katibu Mkuu wa BAVICHA ambaye ni Mwenyekiti wa Kambi ya Mbowe.

*Nani wa kwangu aliyekamatwa?

MY TAKE:
Huyu dada Kijakazi Yunus alipata tabu sana kumhoji Tundu Lissu.

Huyo anayeonekana mwanzoni mwa video hii, mwenye shati refu jeupe na raba nyeupe anaitwa DANIEL NAFTARI. Ni mratibu wa Kampeni za Mwamba Mbowe.
Hapa anafukuzwa na BAVICHA Ubungo Plaza wakimtuhumu kutoa rushwa kwa Wajumbe ili kuiharibu Uchaguzi.

Idrissa Rubibi alivyokutwa Chooni akigawa Rushwa. Akajitetea kwwamba alikuwa anatoa nauli kwa wajumbe kutoka Kanda ya Magharibi.

Swali: Kwanini hiyo nauli asitumie Ofisi hadi akajifiche chooni?
 
Huyo anayeonekana mwanzoni mwa video hii, mwenye shati refu jeupe na rab nyeupe anaitwa DANIEL NAFTARI. Ni mratibu wa Kampeni za Mwamba Mbowe.
Hapa anafukuzwa na BAVICHA Ubungo Plaza wakimtuhumu kutoa rushwa kwa Wajumbe ili kuiharibu Uchaguzi.
View attachment 3204093
Lafudhi za kilugaluga
Wewe usituvurugii uchaguzi wewe.
Asituvurugii uchaguzi.
 
Lissu akiwa anafanya siasa za uongo na utapeli.
Screenshot_20250117-073729.jpg
 
Uyo dada ni mweupe sana,nimeona mpaka Aibu eti usitaje majina hii nchi Ina watu zero kabisa
Huyo dada ni mfano halisi wa upeo wa wana CCM wote.

Kwa akili zake ndogo anaamini kuwa na yeye ana mamlaka kwenye hii nchi zaidi kwa vile ni mwanachama wa CCM.

Sitostaajabu kesho ukasikia ni mkuu wa wilaya kwa kazi nzuri aliyofanya ya 'kumdhibiti' Lissu.
 
Huyo dada ni mfano halisi wa upeo wa wana CCM wote.

Kwa akili zake ndogo anaamini kuwa na yeye ana mamlaka kwenye hii nchi zaidi kwa vile ni mwanachama wa CCM.

Sitostaajabu kesho ukasikia ni mkuu wa wilaya kwa kazi nzuri aliyofanya ya 'kumdhibiti' Lissu.
Hakika usishangae akapelekwa Mbozi kuziba nafasi ya Ester Mahawe kwa ujinga aliouonesha
 
Back
Top Bottom