Watanganyika, Disemba 14, 2014 Ni Hatua Ya Mwanzo Kuiondoa CCM

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,010
Na Rashid Seif – Mzalendo.net

KWA HALI halisi na isiyovumilika kwa nyanja zote za maisha ya watu iliyopo sasa ni lazima watanzania, upande wa Tanganyika, kesho kuanza hatua ya mwanzo kuiondoa CCM.

Watanganyika wote kesho wanapaswa kuanza hatua ya mwanzo kuiondoa CCM madarakani, ni hatua ya awali katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.

Kwa sasa ni sehemu moja tu Tanzania wamefanikiwa kuiondoa CCM kila kona ni kule Pemba. Hakuna asiejua ndani na nje ya Tanzania kuwa CCM imeshaondolewa Pemba, tangu miaka ya 90.(kuanzia uchaguzi wa kwanza 1995) CCM haina Jimbo Pemba.

Serikali ya Muungano ya Tanzania, kwa kutumia JWTZ na Jeshi la Polisi, Serikali ya Zanzibar ya SMZ, nayo kwa kutumia vikosi vyake pamoja na ‘USALAMA WA TAIFA’ wamejaribu kila hali kutaka CCM ibakie Pemba, juhudi zao hazijafanikiwa kurudisha chochote zaidi ya kuzidi kutengwa.

Ikumbukwe kwamba, Rais wa sasa wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ambaye kwa maneno ya mitaani anaonekana kuwa ni MPEMBA, aliwahi kugombea uwakilishi katika Jimbo la Mkanyageni, wananchi walimktaa baada ya kugundua kuwa ni dalali. Ilikuwa mwaka 1995.

Si safari ndogo, safari bado ni ndefu na yenye hatari ila huu uchaguzi wa kesho ni moja kati ya hatua za majaribio ya Umoja wa Vyama vya Siasa (UKAWA) kuhakikisha CCM inapunguzwa nguvu na makali.

Tunaweza tukaamini kuwa kazi ya kuiondoa CCM madarakani ni ngumu kwa sababu bado CCM inasikilizwa na vyombo vya dola, hasa Jeshi la Polisi na hasa Tanganyika.

Lakini hata hivyo, Watanganyika wanapaswa kuigeuza shilingi upande wa pili kama walivyofanya wenzao Pemba, hapa muhimu ni kujiamini kwa kuondoa hofu na woga kama wenzao wa Pemba.

Hakuna Mtazania asiyejua udhalilishaji wa aina zote waliyofanyiwa watu wa Pemba, lakini mwisho wa siku CCM imekufa, ingawa haikuwa kazi rahisi.

Hakuna mwancnhi hata mmoja Pemba, ambaye kwa njia moja au nyingine hakuonja adhabu kutoka serikali za CCM. Wapo waliyo-uawa, waliyo-lawitiwa, waliyopigwa, waliyolishwa vinyesi vyao wenyewe na uonevu mwingine.

Kunahitajika umoja miongoni mwa wananchi kuikabili CCM na kuing’oa, vyenginevyo kama wanavyosema viongozi wake kuwa CCM itatawala milele. Kesho ni siku sahihi ya kuikana kauli hiyo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…