Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,289
- 9,619
Watalaam wa mafuta na gesi Tanzania: Waishauri serikali juu ya ongezeko la bei za mbolea, mafuta ya petroli na dizeli nchini.
Kuhusu kupanda kwa bei za mafuta ya petroli na dizeli, mtaalam wa mafuta na gesi Bwana Elia Wilinasi amesema mafuta ndio nishati inayoendesha injini ya uchumi wa dunia. Bila mafuta uchumi unasimama. Bidhaa zote ambazo zipo kwenye mzunguko wa uchumi au biashara zinategemea mafuta ili ziweze kumfikia mtumiaji wa mwisho. Bei za mafuta ya dizeli na petroli zinapopanda hata bei za usafirishaji wa bidhaa hizo hupanda na kuathiri bei za kununua bidhaa hizo kwa mtumiaji wa mwisho. Hivyo bei za mafuta zinapoongezeka huongeza mfumko wa bei maradufu.
Naishauri serikali ichukue baadhi ya hatua ambazo zinaweza kupunguza bei za mafuta ya petroli na dizeli nchini. Hii itasaidia kupunguza gharama za maisha zinazosababishwa na mfumko wa bei za bidhaa.
Ili kupunguza bei za mafuta ya petroli na dizeli katika kipindi hiki naishauri serikali mambo mawili. Moja naishauri serikali kama inawezekana ipunguze kodi na tozo kwenye mafuta ya petroli na dizeli. Inaweza kuzipitia kodi na tozo zilizowekwa kwenye mafuta na kutoa nusu ya kodi au tozo kwa kila kodi au tozo ili ibaki angalau nusu yake kwaajili ya kukamilisha mipango ya serikali na kuziendesha taasisi zinazotegemea kodi au tozo hizo. Pili, naishauri serikali itafute fedha zitumike kama ruzuku kwenye mafuta ya petroli na dizeli. Fedha hizo ziongezwe kwenye kila lita ya mafuta ili kupunguza bei ya mafuta kwa mnunuaji wa mwisho. Mfano inaweza kuamua kuweka hata ruzuku ya Sh. 500 au Sh. 1000 kwa kila lita moja. Fedha hizo zinaweza kurudi kipindi ambacho bei ya mafuta itakua imeshuka katika soko la dunia.
Kuhusu bei za mbolea kuwa juu, Bwana Elia Wilinasi amesema uhaba wa usambazaji wa mbolea katika soko la dunia unaochochewa na vita vya Ukraine na Urusi umesababisha bei za mbolea kuwa juu.
Bei za malighafi zinazotumika kuzalisha mbolea mfano amonia, naitrojeni, naitreti, fosfeti, potashi na salfa - zimepanda kwa asilimia 30 tangu mwanzoni mwa mwaka wa 2022.
Urusi na Ukraine ni miongoni mwa wazalishaji muhimu zaidi na wakubwa wa bidhaa za kilimo duniani. Mwaka 2021, Urusi ilikuwa muuzaji mkuu wa kimataifa wa mbolea za naitrojeni na msambazaji wa pili wa mbolea za potasiamu na fosforasi.
Urusi, ambayo inachangia karibu asilimia14 ya mauzo ya nje ya mbolea duniani, imesimamisha kwa muda biashara ya kuuza mbolea nje ya Urusi. Jambo hili linasababisha athari kubwa katika masoko ya kimataifa.
Zaidi ya hayo, gesi asilia ni malighafi muhimu sana ambayo hutumika kuzalishia mbolea za kilimo. Nchi za ulaya na Asia ndizo zenye viwanda vingi vya Kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi asilia. Bei ya gesi asilia kuwa juu imesababisha kupungua kwa uzalishaji wa mbolea katika mataifa hayo yanayozalisha mbolea. Kupungua kwa uzalishaji wa mbolea kumechangia uhitaji kuwa mkubwa na bei zimeongezeka sana katika soko la dunia. Bei ya gesi asilia inapopanda hata gharama za uzalishaji wa mbolea nazo hupanda.
Ninaishauri serikali ipunguze bei za mbolea kwa kuziwekea ruzuku ili kuweza kuwapa wakulima unafuu. Lakini pia serikali iweke mikakati ya kupunguza utegemezi wa kuagiza mbolea kutoka mataifa ya nje ili siku za usoni iweze kukabiliana na athari za mabadiliko ya bei katika soko la dunia. Kwani taifa lina gesi asilia, basi liweke mikakati ya kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea kwasababu malighafi zote tunazo.
Naye mtalaam wa mafuta na gesi Bwana Msuya ameishauri serikali kuweka mipango ya muda mrefu ili iweze kukabiliana na bei za mafuta nchini. Moja amesema naishauri serikali ijenge maghala makubwa ya kuhifadhia mafuta nchini. Maghala yaliyopo yanauwezo wa kuhifadhi mafuta kidogo.
Naishauri serikali ijenge maghala makubwa yatayoweza kuhifadhi mafuta ya kutumia kuanzia miezi sita na kuendelea. Mafuta yatakayohifadhiwa yanaweza kuja kutumika kutoa ruzuku nyakati ambazo bei zitakua ni kubwa. Lakini pia naishauri serikali kuendelea kutafuta mafuta ardhini kwaajili ya kujitegemea katika nishati hii muhimu. Kwani kuendelea kutegemea kuagiza mafuta ni hatari kwa uchumi wa taifa. Kwani ipo siku wanaotuletea watagoma kuyaleta kwasababu za kiusalama au kwa kukosekana sokoni. Hii itakua ni hatari sana kwa taifa letu.
Naye mtaalam wa kemia ya petroli, Tumwimike Mwaipasi, amesema naishauri serikali iendelee kupanua matumizi ya gesi asilia ili kupunguza utegemezi wa nishati kutoka mataifa ya nje. Kwani gesi asilia inamatumizi mengi. Mfano Qatar ni nchi yenye hifadhi kubwa ya gesi asilia. Katika nchi ya Qatar, wamejenga kiwanda ambacho kinaibadilisha gesi asilia kuwa mafuta. Mimi nilikua naona pia mbali na kutafuta mafuta ardhini, serikali ingewekeza kwenye mikakati kama hii ambayo ni endelevu.
Mwisho mtaalam wa kemia ya mafuta na gesi, Bwana Hussein Millanga, binafsi nipende kuiomba serikali kuweka nguvu katika kuhamasisha matumizi ya Compressed Natural Gas (CNG) kama njia mbadala baadala ya kutumia mafuta katika vyombo vyetu vya usafiri. Hapa naongelea serikali kuandaa matamasha na semina juu ya faida kubwa iliyo katika utumiaji wa CNG bila kusahau kuwakaribisha wawekezaji kuweka mitaji yao katika biashara hii. Kipekee serikali itende katika hili kwa magari ya mwendokasi yaliyopo katika jiji la Dar es salaam kutumia mfumo huo wa nishati.
Chanzo: Nipashe