Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 732
- 1,470
Utafiti wa kisayansi uliofanywa miaka 12 na watafiti toka Taasisi ya Watafiti ya Wanyama pori Tanzania (Tawiri) imefanikiwa kupata dawa ya Asilia inayosadia kuotesha nywele na kuzuia kukatika kwa nywele.
Taarifa hiyo iliweza kutolewa Jana siku ya jumanne Tarehe 22, April 2025 jijini Arusha, ikiwa ni hatua muhimu katika utafiti wa Tawiri kuhusu mimea yenye dawa iliyo hatarini kutoweka yenye sifa za uponyaji wa asili, ulioanza mwaka 2013.
Dawa hiyo imetokana na magogo ya mti unaitwa mporojo (Albizia anthelmintica), unaoajulikana kama "wormwood" matibabu haya ya nywele yaligunduliwa kwa ushirikiano wa karibu na jamii za wenyeji katika Wilaya ya Ngorongoro, ikiwa ni pamoja na makabila ya Maasai, Hadzabe, Datoga, na Iraq.
Haya ni maendeleo muhimu kwa watu wanaokabiliwa na upara, nywele nyembamba, au kukatika.Upimaji wa kisayansi umethibitisha kuwa Albizia anthelmintica ina mali ya kipekee ambayo inakuza ukuaji wa nywele na kuzuia upotezaji wa nywele," mkurugenzi wa utafiti wa Tawiri, Dk Julius Keyyu.