Wataalamu wa umeme hii inasababishwa na nini?

Vhagar

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
20,342
39,572


Siku ya majuzi jumapili. Sina hili wala lile wakati vitu karibu vyote vya mbele viko on? Radio (av receiver) tv na pc.

Ghafla tu vikazima mara naona moto katikati ya waya wa cable. Haraka nikazima switch ukutani.

Akili ya kwanza nikajua kuna kifaa kishaungua.. Nikatoka kwenda kula then nikarudi nilichofanya nilikata lile eneo lililitokea hitilafu kwa mkasi then nikaunganisha tena. Halafu nikawasha tena. Ila kila kitu kilikuwa poa tu. Hakuna kifaa kilichokuwa kimeungua labda.
 
Nunua Tronic achana na power supply za kiboya hizo 🤣
 
Mkuu, unajua humu JF ni darasani, hiyo Tronic ni nini na inafanyaje kazi... twende darasani...
Hio power extension cable ambayo imeungua hapo pichani ni fake na ya kichina. Huwa inafungwa na waya laini ambazo hqziimili mikiki ya umeme wetu wa kibongo ambao ni unstable. Ukizidi kidogo tu nyaya zinayeyuka na kugongana ndio moto unawaka kama hivyo.

Nenda dukani waambie unataka tronic ni ghali lakini imara. Something like TZS 18000 au juu kidogo kulingana na unataka ya njia ngapi.
 

Tronic Ulumbi mwingi ,Konki ila bei imechangamka sana ,Tundu 6 nadhani kama 25 mpaka thalatha.

Hizi za kina Hujintao ,Xi Jing Ping buku 5 tu ila ndiyo Snura Majanga.
 
Zingatia ya wadau apo... chapili zingatia Power consumption rate ya extension zako sio extension ipo rated 5A nawewe unachomekea pasi ya 13A maana yake inazidiwa na lazima iungue.... vitu vinavyo draw umeme mkubwa kama pasi, rice cooker, na majiko ya umeme ikibidi uchomeke kwenye socket kabisa na kama ni nyumba yako wakati wa wiring mafundi wavutie waya wa jiko ikiwezekana 6.00mm² na uiekee socket maaulumu kwa jiko
 
Hili ni tatizo kwa watu wengi sana kwenye nyumba zao. Fuatilia hapa chini..
Waya wowote, huwa una uwezo wa kubeba CURRENT kiasi fulani kwa kiwango cha juu. tazama jedwali hapa chini



Extension cable nyingi ni za 1.5 au 2.5 square millimeter na chache sana ni za 4 square millimeter (Cross section area) na ni home made

Wengi wetu, tuna extension cable za 1.5 square millimeter tunazonunua dukani. Wakati tunachomeka vifaa kwenye extension cable, huwa hatuangalii tunachomeka kifaa chenye kuhitaji current kiasi gani, na hatuangalii tunachomeka vifaa vingapi kwenye extension cable moja.

Hebu fikiria, umechomeka pasi ya umeme yenye power ya 2kW, kwa 220V, hapo unazungumzia 9A. Halafu extension cable hiyo hiyo iwe na TV, Radio, etc HALAFU UKUTE NI 0.9 sqr mm huku imeandikwa 1.5 sqr mm. Na wengine mnachomeka pasi mbili kwa wakati mmoja kwenye extension cable moja.!!!

Kwa kawadia, waya wowote una resistance (ukinzani) ambayo kwa kupitisha current kwenye waya huo, joto hutokea. Sasa ukubwa au kiwango cha joto hutegemea kiasi gani cha current kinapita kwenye waya huo. Kiwango cha joto, kikifikia joto la kuweza kuyaunguza magamba (insulation) ya waya, moto hutokea kama ulivyooneka kwenye picha yako.

Waya zipo kwa standard kwa maana ya size. Lakini kwa bahati mbaya, watengenezaji wengi huwa hawafikii starndard hiyo. Utaandikiwa waya ni wa 1.5 sqr mm lakini kiuhalisia ni chini ya hapo.

KUZUIA HAYO, HAKIKISHA UNA SWITCHED SOCKETS ZA KUTOSHA KWENYE NYUMBA YAKO ILI KUPUNGUZA MATUMIZI YA EXTENSION CABLES NYUMBANI KWAKO.
 
Asante sana mkuu, umefafanua vyema sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…