Wasomi na ndoto za Abunuasi

bhunonukid

Member
Jul 3, 2016
11
18
Hebu vuta picha,namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule.Umekumbana na kashkashi za walimu "wanoko",ukiwaona tu bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda.

Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.
Ukupigao ndio ukufunzao,ila hukujifunza pale ulipochaguliwa chuo!
Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat screen, "dance floor" vikahamia chumbani kwako!

Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako!
Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda wa kula "pensheni" mana msomi umeshavaa joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti!Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na "vizenga"(vibomu).Ulijulikana kama mzee wa "kujilipua".

Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo.Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowacha ambao hawakuendelea na masomo, wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye biashara zao!

Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu!Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali!

Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu!Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma "Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?ndiyo uko maabara sasa.

Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata" chuoni,lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza kuisoma namba" !Umepauka kama koti la mtunguo Tandika!
Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya 1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na "demu" mkali,zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni!

Magari unayaona mjini tu,"mademu" wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti za kupauka kama inzi wa chooni. Gucci unaziona kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni tu!

Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani "vascoda Gama", baada ya shida kukutandika vibao,sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo na kupata kazi utaunga kusoma masters?Vipi kwani vyuo vimefungwa?

Haya ndio maisha ya vijana wengi! Hudhani mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite!Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi,kucha feki na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake.

Nguo ya ijumaa hufuliwa Alhamisi #JIPANGE jombaaaaaaaaaa m
Nimeipata sehemu
bora nishee nanyi maana Kuna wanafunzi humu so ukipata boom yako jua Kuna kilimo na ufugaji baadae
 
Ukiwa mwaka wa mwisho chuo au ukimaliza, find your passion. Iwe ni kazi au wazo la biashara. Kama ni kazi usikimbilie kazi ya aina yoyote, nenda kajitolee kwenye kampuni inayofanya kazi zinazofanana na aina unayoipenda. Na kama ni biashara anza taratibu, sota mtaani kwanza upate akili.....kula mlo mmoja kwa siku na pia demu wako wa chuo akutose coz huna hela...hapo automatically utakua unajitengenezea emotional intelligence au killer insticts au njaa ya mafanikio ambayo utaishi nayo siku zote. All the best bro
 
ukikaa na wanachuo utawahurumia jinsi walivyo na ndoto za kumaliza chuo na maisha kua kama ya messi vilee,yani ni fulu ndoto za abunuasiii.
sio mbaya kwa mtu kuwa na ndoto zake hata kama hazitakuja kutimia. kila mtu ana namna yake ya kuja kujifunza katika maisha..................
 
mkuu, huu uandishi umekaa kuzodoana sana kuliko kuelimishana................................
 
Ila kuna ukweli ndani yake lkn namna ya kujifunza maisha na kutafuta pesa njia zinatofautiana so ulivyo pata ni tofauti na wengine watakavyo pata
 
Nimeipenda hii, na kama ni lugha basi kwa mimi nasema umetumia lugha ya kisanaa(utani) kufikisha ujumbe .
 
Mimi nina mtazamo tofauti....ukiwa unakaribia kumaliza chuo ni kujiamini tu kwamba mambo yatakua poa...kazi utapata..(na ujue jinsi ya kutafuta kazi) haijalishi kozi uliyosoma kazi zipo....sema kutafuta ndo watu hawawezi...watu wengi ni wazito....hata umwambie kuna post nimeiona itakufaa atakuitikia fresh nitaicheki....
 
Kuna watu huwa mnaboa hivi mnazani hyo hela ya boom mtu unweza ukaisave kweli. Hela yenyew laki mbili na nusu kwa mwezi umepanga mtaani kodi elfu 40 hela ya maji elfu 5 kwa mwezi, hela ya umeme ni elfu 30 kwa mwezi unataka huyu mtu a save hyo hela inatoka wapi,? Unakuta hapo uba mdogo wako yupo a level na yeye anakuomba hela ya matumiz kwenye hyo hyo laki mbili na nusu.
Ukiona mtu anatumia hela ya boom kwa starehe ujue ana back up kwa wazazi
 
Kweli boom ni ndogo sana
 
tupe ushaur bac
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…