Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 355
- 769
Imefika wakati sasa Tanzania inabidi tuliangalie tatizo la ajira kwa jicho pevu maana hili bomu karibu linalipuka. Idadi ya degree zinazotoka vyuoni kila mwaka ni namba inayotisha ukizingatia huku mtaa unahitaji performers not graduate.
Huku mtaani boda boda karibu wote ni degree holders, achilia mbalimbali makondakta na wezi pia wote ni wasomi. Tanzania turudi sasa kwenye misingi ya kweli ya kulikomboa taifa kiuchumi kwa kijikita zaidi kwenye teknolojia, ufundi, ubunifu, kilimo na kuzingatia upatikanaji wa mitaji kwakua bila mitaji bado kila kitu ni zero.
Tujiwekeze kwenye uzalishaji wa mahitaji yetu ya ndani kwanza, tukijitosheleza, tunaanza kuhudumia na majirani zetu.
Tazama china ilivyo sasa, tunachokiona china ni matokeo ya nia ya dhati ya viongozi wao tangu kuwekwa misingi ya taifa lao, commitment na uchapakazi, Leo china inahudumia karibu Dunia nzima. Nini utahitaji kutoka china ukose, kwanzia soksi, Pini, viberiti magari mpaka vijiti vya kutoblewa meno.
Je ni kweli Tanzania hatuwezi kutumia pamba yetu kutengeneza nguo "made in Tanzania"?
Soma Pia: Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri
Je ni kweli kuwa kufufua kiwanda cha Mwatex, Mutex, Kili tex, Sungura tex na general tire ni mission impossible " hivi viwanda peke yake tu vinahuitaji wa vijana wangapi wanaoweza kuajiriwa hapa?
Je ni kweli kwamba Tanzania hatuwezi kutumia rasilimali zetu kama madini kutengeneza vifaa muhimu vinavohitajika duniani kama ilivyo madini ya cobalt na mengineyo yanayotumika kuendesha vifaa vya umeme kama iphone, laptops na simu.
Tiss haya ni majukumu yenu kuongoza harakati za kijajusi kukomboa nchi kutoka na hili janga.
Tuingie ubia na makampuni yatakayotuuzia teknolojia na kuhakikisha viwanda vinafunguliwa Tanzania Ili kutengeneza ajira. hamasisheni ubunifu na kutoa kipaumbele kwa kila wazo au ubunifu wenye manufaa.
Kiufupi tunatakiwa tufanye
1: Uwekezaji katika Sekta za Kimkakati: Sekta kama kilimo, utalii, nishati, na viwanda vinaweza kuanzishwa au kuimarishwa zaidi ili kutoa nafasi za ajira nyingi. Uwekezaji katika miundombinu ya nishati na usafirishaji pia unaleta fursa za ajira.
2: Kuboresha Sheria na Mazingira ya Biashara: Serikali inaweza kurekebisha sheria na taratibu ili kuboresha mazingira ya biashara. Hii itavutia wawekezaji wa ndani na wa kigeni na kutoa fursa za ajira kwa wananchi.
3: Kukuza Sekta ya Teknolojia na Ubunifu: Maendeleo katika teknolojia na uvumbuzi yanaweza kuongeza ajira kwa vijana. Kupitia program za mafunzo ya teknolojia na ujasiriamali wa kidigitali, Tanzania inaweza kuongeza idadi ya ajira katika sekta hii.
Tuache ku play politics kwenye maisha ya watanzania, kama Kuna nia ya dhati, serikali ikae chini na Baraza la vijana Tanzania, kuweka mikakati sahihi na serikali kuheshimu na kutekeleza hatua zote muhimu Ili kuona malengo ya kujikwamua kiuchumi kama taifa yanatimia.