Nimeshangazwa Na hao wanaojiita Wasomi Kwa kuilaumu Kambi ya Upinzani Bungeni kuwa Bubu katika mijadala ya bunge.Nilitegemea wasomi hao wangekuwa wa kwanza kukosoa mwenendo mzima wa bunge unavyoendeshwa.Tumeshuhudia Spika anakiuka taratibu Na Sheria za bunge toka upangaji wa kamati za bunge Kwa kuzipanga Kwa upendeleo Na matokeo yake tumeyaona wabunge wamekuwa wala rushwa.Kuna kamati mbili ambazo ni lazima ziongozwe Na Upinzani lakini Spika amekuwa ana kiuka taratibu .Tumeshuhudia bunge Kwa kushirikiana Na Serikali zinakandamiza Uhuru wa watanzania kupata habari Kwa kuzuia kutushwa Kwa matangazo ya bunge moja Kwa moja ili wananchi wawaone wawakilishi wao wakichangia kile walichowatuma.Tumeshuhudia serikali ikibadili matumizi ya fedha bila kupata idhini ya bunge kama Sheria inavyotaka hata kama ni Kwa manufaa ya wananchi lakini Sheria in lazima Na bunge limekaa kimya.Na mwisho bunge lenyewe limehamisha fedha bila wabunge kujulishwa Na kupitisha.Nilitegemea hao wasomi Dr.Bana hayo yote angeyasemea kuliko kuulaumu upinzani Kwa kukaa kimya .Upinzani umeamua kukaa kimya kwani Sheria Na taratibu zinakiukwa wasomi wetu mko kimya wao upinzani kukaa kimya ndio kina Dr.Bana mnajitokeza kulaumu mbona hamjitokezi kuhoja uvunjwajiwa katiba Na Sheria unaofanywa Na Serikali Na Bunge hamhusemei?Mbona wananchi kukosa matangazo ya bunge Live mmenyamaza? Wasomi wetu acheni unafiki kwenye mambo ya manufaa Kwa Taifa letu.