Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,273
- 21,455
Ni swali ambalo sasa liko vichwani mwa watu wengi tu. Biashara ya pembe za ndovu duniani kimsingi imepigwa marufuku. Hadi sasaTanzania ndio inaonekana kuwa na ghala kubwa mno la pembe za ndovu duniani, zinazokamatwa toka kwa majangiri na tembo wanaokufa wenyewe. Nchi kama Kenya huwa wanazichoma moto pembe kama hizo.
Tanzania imekuwa mstari wa mbele kutaka kuuza pembe zake kihalali, na imeambiwa hilo haliwezekani. Kila inapoomba kuuza inakataliwa. Na Tanzania ikiambiwa itoe hesabu ya pembe tulizonazo kila mwaka kulingana na taratibu za kimataifa - inakataa kutekeleza agizo hilo (kwa kuwa zikipungua tutaulizwa zimeenda wapi?)
Sasa watu wanajiuliza, ikiwa tunajua hatuwezi kuziuza pembe zetu kihalali, na hatutaki kuzichoma, na hatukubali kutoa hesabu ya pembe tulizo nazo kila mwaka, je, kama nchi, tunajihusisha na biashara haramu ya pembe za ndovu?
Soma article ifuatayo.
Tanzania on the spot for not making its ivory inventory public