Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,965
- 5,343
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewaonya wanachama wa chama hicho kuhusu umuhimu wa kuchagua wagombea wanaokubalika na Wananchi katika uchaguzi ujao, Oktaba 2025. Akisisitiza kuwa viongozi ni wa watu na lazima wakubalike na wapiga kura ili washinde.
"Tutafute Wagombea Wanaokubalika, Hawa ni Viongozi wa Watu, Lazima Waongoze Watu Ambao Wanakubali", akifananisha anguko lake kisiasa na penzi la mke wa tajiri kwa dereva bodaboda.
"…mtu mwingine anasema wako wangapi nikiweka bilioni tatu, wao wanafikiri kila kitu kinauzwa hakuna, siyo kweli mbona mapenzi hayauzwi na nyinyi mnayajua hayauzwi, ndiyo maana unaweza kukuta tajiri kanyang'anywa mkewe na dereva bodaboda sasa nani ana hela? Siyo kila kitu kinauzwa duniani", ameeleza.