Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,447
- 3,760
Watu wasiojulikana wametekeleza tukio la mauaji kwa kumuua Isack Mallya (72) mkazi wa Kijiji cha Umbwe Onana, Kata ya Kibosho Magharibi mkoani Kilimanjaro na kisha kutelekeza mwili wake nje ya nyumba yake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya Disemba 2, 2024 na kwamba wanafuatilia kujua waliohusika na mauaji hayo.
"Ni kweli kumetokea tukio hilo la mauaji, ambapo huyu mzee amepigwa na kitu kizito kichwani, tunafuatilia tukio hili ili kuwabaini waliohusika na mauaji haya," amesema Kamanda Maigwa
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi ambaye ni ndugu wa Marehemu ameeleza kusikitishwa na ukatili aliofanyiwa kaka yake na kusema wameliachia Jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kubaini waliohusika na sheria ichukue mkondo wake.
"Huyu ni kaka yangu, ni mtoto wa baba yangu mkubwa, tumeishi wote mji mmoja na mahali alipouawa ndipo nimekulia hapo, ni jambo la kikatili sana limefanyika katika jamii, lakini naamini jeshi la polisi litafanya bidii kuchunguza matatizo yaliyotokea na kuwatafuta waliohusika na jambo hili ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake", amesema Boisafi.
Aidha amesema kitendo kilichofanyika hakikubaliki katika jamii na kinatia hofu kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kwamba hata kama walikuwa wanamdai wangesema walipwe kwa kuwa hakuna kitu chenye thamani ya uhai wa mtu.
Akizungumza na Jambo TV, mmoja wa wananchi wa Kijiji hicho ambaye pia ni mwanaharakati, Vicky Massawe amesema tukio hilo ni la kusikitisha kwa kuwa marehemu alikuwa ni mtu wa watu katika Kijiji hicho.
"Huyu baba alikuwa ni mchangamfu na kila mtu hapa kijijini na alikuwa hana shida na mtu, sasa leo asubuhi tunaambiwa mwili wake umekutwa nyumbani kwake nje ukiwa na majeraha na damu zikivuja sana, huyu mzee kauawa kwa mateso sana," amesema Vicky
Chanzo: Jambo TV