Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 14,987
- 31,239
Wengi wao wakiwa na umri wa miaka 18-25 huwavutia wanaume wengi kwa ajili ya Ndoa ,lakini wao huwa hawapo tayari kuolewa kwa sababu mbalimbali
1. Umri wangu Bado mdogo kuolewa
2. Kwa sasa Bado nahitaji kuendelea kusoma
3. Nataka nitafute kwanza pesa zangu
4. Ndoa zenyewe zimejaa matatizo,sihitaji kuolewa
5.Nahitaji uhuru wangu Sio kwenda kuchungwa chungwa na mwanaume
6: huwa na kundi la wapenzi kwa ajili ya kula bata ,haoni shida ,kuwa nao 4 Kila mtu na jukumu lake. Wa Kodi,kula,bata,kuvaa nk
Umri wa miaka 25_30
Huenda tayari kahitimu chuo,kapata kazi au ana biashara zake ,ama mambo yameenda hivyo sana yupo na wazazi wake nyumbani ndipo maswali huwa mengi toka kwa wazazi na ndugu
1. Ina maana Bado huna mwanaume wa Kukuoa?
2. Umri hausimami tafuta mtu akuoe.
3. Basi tafuta hata mwanaume uzae nae tu.
4. Badilisha mfumo wa maisha yako,acha hizo nguo fupi,kwenda kumbi za starehe ,unatakiwa upate bwana uolewe
5. Sawa una pesa unaweza jihudumia lakini tafuta ndoa ikuheshimishe
6. Mwamposa atakuwa na mkutano wa siku 5 hebu uwe una hudhuria unaweza funguliwa ukapata bwana wa kukuoa
Baada ya kufika miaka 30_na kuendelea
Hapa huanza kuwaza na kuwazua nini kifanyike Baada ya ndugu na rafiki wa umri wake wengi wameolewa. Kwa sasa nae anaitamani ndoa
1. Mkrisito huanza kuhudhuria mikutano,kwenda Kila ibada,.muislamu huanza kufunga na kwenda msikitini tofauti na siku za nyuma
2. Huanza mahusiano hata na mume wa mtu ,yupo tayari kuwa hata mke wa pili
3. Aliye kuwa mkali na mwenye dharau akiombwa namba,sasa hivi yeye ndio hutoa namba
4. Huamua kuingia kwenye makundi ya mitandaoni kutafuta marafiki au wapenzi watakao kuwa wapenzi Kisha ndoa
5. Hupunguza vigezo vya mwanaume anae muhitaji,ndo husema Ili mradi anapumua. Wakati mwanzo alisema anataka awe mrefu,mweusi mwenye pesa au kaz nzuri
KUMBUKA
Mungu hupanga hatima ya Kila mtu kwa wakati wake,hivyo unaweza umia sana kumbe wakati wako Bado.
Umri Sio kigezo kuoa au kuolewa muhimu uwe na mtu sahihi. Bora uchelewe umpate mtu sahihi kuliko kuwahi ukamie
Kuna wanawake wapo safi tangu wajitambue ila hawakubahatika kupata wenza sahihi,hivyo bado wanasubiri
Kuna wanawake walipata wenza sahihi lakini wao walikuwa na mambo mengi, saiz wanatamani siku zirudi nyuma wafuatwe tena Ili waolewe
Ukimpata mwanaume au Mwanamke sahihi basi fanya kutimiza ndoto yako ,
.
Kila kitu Kina mwisho
Upweke wako una mwisho pia
Maumivu yako yataisha pia
Kuwa tayari wakati wowote