Wasanii wa Tanzania jifunzeni kustaafu, bongo mziki bado sio biashara ya kudumu

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
10,869
14,273
Salaam!

Ushauri kwa wale wanaojiita ma-regendary wa bongo wakuu ukweli huu hamtaupata popote na auonaye amwambie mwenzie ,wakuu Game ya bongo ya Muziki na hata sanaa zingine sio kazi au biashara ya kudumu ,mtawafariji ooh mbona wa ulaya mpaka leo wanapiga show ,wakuu hilo game la ulaya leo hii hapa bongo huwe andaa tamasha la Prof J,mr 2, J Nature eti sisi mashabiki wao enzi hizo tukajae ukumbini wengi wetu tuko na familia ,tumetingwa na kazi na biashara huo muda wa kwenda Diamond jubiree haupo.

Nimesikiliza sana intervie za dudubaya,dullysykes ,TID ,PROF J yaani wanaongea kama bado wanayo nafasi aliyonayo leo mbosso kuwa vibao vikali vinakuja TMK et nao wanazungumzia kupata manager ,nani tena anasikiliza nyimbo zao?

Malegend mkubali zama zenu zimepita kwa sasa pambaneni na maisha mengine ,oneni mtu kama mwana fa au ay tukiachana na lile zali la kesi ila kitambo walijikita biashara zingine ,ila ukiona anahojiwa inspector haroon yaani ni kama ana ndoto kuwa iko siku atajaza ukumbi,mashabiki unaoona wanajaa show za alikiba na Diamondi age yao ni 14 hadi 25 kuanzia 26 kijana anakuwa kabanwa na makodi ya nyumba stress za waliyezaa naye ,ndoa,na kwa wadada zetu 26 anakuwa aidha busy na biashara familia yake au mdangaji wa kuvizia wazee huo muda wa kwenda show anatoa wapi.

Wakuu malegend tunawapenda ila kuweni kama nooray aka baba staz alijisoma mapema yuko busy na kuuza spea na anaendelea vyema kabisa .au wote mtaishia kama chidi benzi mpaka leo analalamika anataka collable ya Diamond wakati style zao zimeshakufa na mashabiki wao halisi sisi ambao saivi natype nikiwa na mtoto anaumwa nimemuacha wodin huo muda wa kwenda show ya alichoki nautoa wapi .
 
We
Wewe kwenye kazi yako umeshastaafu?
 
Hapo kwenye mdangaji wa kuvizia wazee😅😅
 
Uko sahihi. Hata huko Ulaya ni wakongwe wachache ambao bado wako active. Muhimu kwa msanii kujipanga.
 
Uko sahihi. Hata huko Ulaya ni wakongwe wachache ambao bado wako active. Muhimu kwa msanii kujipanga.
 
Huoni AY na lile kundi lake la mchongo la Samia Kings anavizia vizia teuzi za KICHAWA
Siasa za bongo uwe na timing, hao kina AY sidhani kama watalamba teuzi yoyote zaidi ya kula hela za mama.
FA, Keysha na yule kidoti walipotea kidogo kwenye usanii wakaja kuibuka ni ccm kindakindaki, huko underground walikua wanapiga harakati kimyakimya.
 
Kuna wasanii ambao mfumo umewakataa labda kutokana na aina ya muziki waliouimba lakini kuna wengine huwa ni timeless tu. Waondoke warudi, bado nafasi yao ipo solid mfano

Mwana FA ambaye hajawahi kuchuja, kuna Ray C, Dully Sykes, Lady Jay Dee (huyu yupo active lakini anastruggle kutengeneza hits) etc

Lakini kingine wangefanya show za heshima kama lady jay dee, yeye hajali hizo fiesta ama wasafi festival. Anatengeneza show zake very classic na huwa anajaza. So issue sio kurudi juu Ila kulielewa soko lako na kulilisha. Kuna wengi tu late 20's, 30's hadi 50 ambao wanahudhuria show so usiiweke kama vile, legends hawana watu. Wanao pia
 
umeongea ukweli mchungu sana, kwa ma broo wa muziki wa bongo fleva ambao walitamba zamani na hata sasa. wajitafakari mapema wafanye mambo mengine ya kuwapatia kipato cha kudumu, kwa fedha walizozipata ktk muziki. uwekezaji k.v REAL ESTATE ungewafaa sana kwa maisha yao yote.
 
Legend mwingine nimetoka kumsikiliza Jana yaani ushauri mwingi Kwa wasanii wa sasa alafu ndani ya mwaka Mmoja ametoa singles kama 3 na zote zimebuma🤣🤣🤣
Wakati ukuta ukishindanao utaumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…