Wasanii Roma, Nay wa Mitego na nusura ya kifo

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
140
575
WASANII ROMA, NAY WA MITEGO NA NUSURA YA KIFO.

Ilikuwa alfajiri majira ya saa 10, nikatoka ndani ya Ukumbi wa Silver Sand uliokwepo pembezoni kwa bahari ya Hindi nikaelekea hadi nje ya geti ili kukwepa makelele ya muziki ndani na kupata wasaa wa kuongea na Msanii Nay wa Mitego aliyechelewa kufika kutumbuiza kwenye tamasha la kuwakaribisha wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Daah kumbe huko nje ya geti nilienda kukitafuta kifo bila kujua....!!

Nitangulize kusema mimi Suphian nimewiwa kuhadithia hili tukio kama sehemu ya kusherekea Mwezi wa Septemba ambao ndio nimezaliwa. Matukio ninayo kadhaa ya kutishia uhai wangu kama ambavyo naamini wengi wetu tunayo ila hili SITOLISAHAU. Ingawa ni ndefu ndefu ila mjitahidi kuimaliza kusoma kama jambo utajifunza na kuburudika pia.

Stori inaanza nipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa Pili karibia miaka 10 iliyopita. Chuoni zaidi ya Mwanafunzi, pia nilikuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanafunzi iitwayo DUTTSO (niliyoianzisha) iliyohusika na kukuza vipaji na kupashana habari na pia nilibarikiwa kuwa Mtangazaji na Mzalishaji wa Kipindi cha MUZIKI na MAISHA kilichomulika maisha na kazi za wasanii wa muziki kilichokuwa kinarushwa Mlimani TV.

Kofia hizi mbili (nitazielezea kiundani siku nyingine) ndizo zilizonifanya nifahamike ndani na nje ya viunga vya Chuo kama Mdau Mkuu 'Star' wa Burudani, na hivyo kupelekea almost kila mtu au Taasisi iwe ya Wanafunzi au ya Wanajumuiya wengine wa Chuo, au wadau wengine wa nje wenye interests ama matukio ya Burudani kunishirikisha ili niwape sapoti kwa namna mbalimbali ikiwemo CONNECTION (Ila sio ile ya akina Mama J haha ha (joke).

Kama ilivyokuwa kawaida UDSM kila mwaka, Serikali ya Wanafunzi, DARUSO huandaa matamasha ya kuwakaribisha Wanafunzi wa mwaka wa kwanza, maarufu kama "Welcome First Year", basi nilitafutwa na kupewa 'dili' la kuwatafuta na kuwasimamia wasanii wa kukonga nyoyo na kuwa mshika kipaza sauti (MC) siku hiyo.

Kwakuwa dili hizo zilishazizoea, hivyo sikufanya ajizi, nikaangalia wanamuziki wanaowika na kupendwa kwa muda huo (kama nilivyosema nilikuwa nawahoji), hivyo haikuwa kazi ngumu- nikawatafuta na kukubalina na wasanii Linah, Sam wa Ukweli (RIP), Nay wa Mitego pamoja na Roma Mkatoliki ambaye tulikuwa tunasoma nae mwaka mmoja hapo Mlimani (UDSM) yaani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Siku ikafika bana, nikajikoki tisheti nyeupe, suruali nyeusi na GUCCI (ya wakati huo) mguuni... (Kama ninavyoonekana pichani). Basi nikatimba viwanja vya Silver Sand mapema jioni, shughuli ikaanza kama saa 3 usiku hivi... Yaani mida kama ya saa 5 wasanii wangu Linah na Sam wa Ukweli walishafika hivyo kama MC nikawakaribisha wakapiga show kali sana.

Roma na Nay hawakuwahi mapema kwasababu wao niliwapanga wamalizie show, na ikumbukwe show ilitakiwa ikome majira ya 'majogoo'. Hivyo Dj akaendelea kupiga 'Ngoma kwa ngoma' . Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza na sisi wengine tukaendelea kulifaidi jiji la Dar huku tukipata upepo mwanana wa bahari ya Hindi. Si unajua wengi tumetoka mikoani... hivyo ilikuwa time ya ku-experience the difference..na kuyafurahia maisha ya Chuo.

Mishale kama ya saa 8 usiku nikampandisha rafiki yangu Roma Mkatoliki akachana sana hapo na alikuwa wa 'moto' sana, si unajua ni mwanafunzi mwenzenu halafu alikuwa si mtu wa kuonekana yaani adimu ndio maana wengi waliosoma nae hawakumjua kwa sura ingawa nyimbo zake za kuikosoa Serikali ya Rais Kikwete zilikuwa zimeshika kasi kwa redio ila sio TV kwani alikuwa hajaanza kutoa video.

Roma Mkatoliki alipomaliza, ikabaki 'mchizi' wangu Nay wa Mitego. Nilimpigia simu muda karibia wote alisema yupo njiani, cha kushangaza simwoni na kwenye poster aliandikwa yupo, Wanafunzi wanamuulizia na wakati huo naye anatisha na nyimbo zake zile za 'vichambo' hahah

Muda ulizidi kusonga, ikafika saa 10 alfajiri (si mnajua ukiwa kwenye Starehe za muziki muda unakimbia balaa), nikaanza kuhisi kuchanganyikiwa kumbuka advance nilishampa, hivyo nikaamua kutoka ndani ya Ukumbi hadi nje ya geti ili kumpigia kwani kulikuwa na makelele tusingesikilizana.

Kufika tu nje nikakutana na watu mbalimbali wamesimama kwa makundi, wengine Wanafunzi wanaanza kurudi Chuo, na wengine raia tu wa kawaida ikiwemo watu wa usafiri.

Nikanyenyua simu kumpigia Nay, akapokea ila akaniambia amepata ajali njiani hivyo anapambana kupata tiba, ile naendelea kumhoji kupata taarifa zaidi na tuone namna ya kumsaidia, hamadi bin vuu simu ikanyakuliwa mithili ya kifaranga kwa mwewe.... Daah!!

Nikajua tu huyu ni kibaka. Nikapata hasira sana maana nilijua nitapoteza si simu tu, bali namba za watu muhimu na pia kuharibu miadi na watu wangu muhimu. Ikabidi nimkimbize aisee...

Ikumbukwe hiyo beach ilikuwa imezungukwa na pori, so jamaa alikimbilia porini, na kwakuwa UMITASHUMTA na UMISETA hukunipita kushoto kwenye riadha, nikamkimbiza, nikampiga 'ngwala' yaani mweleka, akadondoka na kuamka, tukaingia porini,... na bahati nzuri kulikuwa na mbalamwezi. Kilichotokea huko, nikiwaza hadi sasa moyo unaenda mbio loh!!

Nilifanikiwa kumkamata, nikampiga ngumi za kutosha kadondoka, tukagarazana hapo chini, jamaa hataki kuiachia simu.. nikamng'ata vidole kidogo vikatike, hadi Meno yangu yalilegea lakini jamaa kaing'ang'ania simu kama ruba. Noma!!

Tukiwa tunaparangana hapo chini, ghafla vijana wakaja kama wanne wengine, nikawaambia mwizi huyu hapa nikijua ni wanafunzi wenzangu wasamaria wema wamekuja kunisaidia. Jibu nililopata kutoka kwao ni ngumi ya ujazo wa Mwakinyo, hakika niliziona nyota kama zoteeee.

Sijajiweka sawa, ngumi, mashuti na vibao mfululizo zilinipata bila huruma, ikanibidi nijibu mapigo, nikarusha ngumi zikawapata kadhaa ila wote walizidi kunivamia, na awamu hii wakawa wanazijumlishia ngumi na viwembe na visu. Nikadondoka kiatu changu kimoja wakachukua. Yaani hapa nililiona kaburi langu kabisa, nguvu ziliniishia, nikaanza kushindwa kuona vizuri maana damu zilichuruzika usoni na kutoka kichwani.

Kifo nilikiona. Nilimwomba Mungu aninusu, Mungu alinisikiliza, alinijaza nguvu za ajabu. Niligeuka mbogo. Nikiwa katikati yao nilinyenyuka ghafla na kuwasambaratisha wote kwa mikono yangu, na kuwadondosha. Nilipata upenyo wa kukimbia.

Nilielekea getini nilipoporwa simu, nilikuwa hoi mno, nikiwa na kiatu kimoja, na mfukoni nikiwa na lako 5 maana hawakufanikiwa kuzichukua. Nilihisi kizunguzungu na kudondoka kama nazi mnazini au pama kutoka mpamani (Wanasingida wananielewa hapa). Wanafunzi walikuja kunikagua wakanijua, maana of course nilikuwa maarufu Chuoni na punde tu nilitoka stejini kama MC, nakumbuka mabinti walianza kulia na kupiga mayowe maana nilikuwa sitamaniki, damu kila pahala.

Moja ya Wanafunzi ninayemkumbuka aliwahi kuja hapo alikuwa anaitwa Marcel. In a minute, watu walijaa. Akiwemo rafiki yangu Msanii Roma. Roma hakufikiria mara mbili aliagiza gari alilokuja nalo linibebe, nikabebwa yeye akiwepo na baadhi ya Wanafunzi. Hapo nilipoingia tu kwenye gari 'nilizima' hadi baadae asubuhi ambapo nilikuja kuahidhithiwa nilipelekwa hospitali ya IMTU iliyopo maeneo ya Mbezi Beach.

Huko IMTU nilipatiwa huduma za kwanza, ikiwemo kusafishwa damu na kushonwa inapotoka. Haya nilihadhiwa nilipopona.

Asubuhi ya siku hiyo nadhani kama saa 4 hivi nilishtuka nipo kwenye gari, watu wanaongea. Niliwasikia akiwemo Roma Mkatoliki. Ilikuwa ni Ambulance. Imagine niliogopa kutoa macho, niliogopa kwani nikidhani nimekufa, so nikaomba iwe ndoto. Ila hakika nilikuwa hai. Nilipelekwa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Hapo hospitalini nilikuta Wanafunzi wengi wananisubiri. Habari zilishaenea Chuo kizima. Humo ndani nilishonwa pia baadhi ya majeraha na mengine yakabaki.

Nakumbuka Dean of Students (Mlezi wa Wanafunzi) Chuoni hapo Prof Qorro alikuja. Akanihoji kwa upole sana, nikamweleza kwa ufupi na kwa shida sana. Akasema nifanyiwa transfer 'uhamisho' kuhamia Hospitali ya Kairuki kwa matibabu zaidi. Na kwa gharama za Chuo. Aliniaga na wanafunzi wenzangu, pamoja na walimu wangu.

Safari ya kwenda Kariuki na Ambulance ilianza Roma Mkatoliki nikiwa nae, pamoja na Girlfriend wangu (wa wakati huo) aliyeitwa Joyce Kombe. Ambaye hakuwa kwenye show ila baada ya tatizo kutokea alitaarifiwa na Roma kwani kuna siku kabla ya show nilimpigia kwa namba yake ili kwenda kumpa fedha ya advance. Girlfriend wa sasa naomba uwe na utulivu ha ha ha

Kariuki nilipokelewa na matibabu yalianza haraka iliwemo kushonwa vidonda kichwani, masikioni, usoni, kifuani, mgongoni na sehemu zinginezo. Roma siku hiyo nzima hakuniacha, alikuwa pembeni yangu akiwa na Mpenzi wangu Joyce. Tulilala. Kesho asubuhi Roma akaniomba ruhusa kwenda Mbeya kwenye Show. Nikamruhusu. You can imagine huyu jamaa alivyokuwa mnyenyekevu na aliyejaa Utu.

Huduma ziliendelea. Yaani Kairuki ilikuwa zaidi ya Hospitali (sijui sasa). Madaktari na Manesi walikuwa wananilea kama mtoto. Nilihudumiwa haswa. Muda wote hawabanduki chumbani kwangu.

Roma licha ya kwenda Mbeya, hakuacha kunijulia hali kila siku kupitia simu ya mama la mama Joyce ambaye nae nilishinda nae hadi nilipopona kabisa. Joyce alihakikisha nakula chakula kinachofaa wakishirikiana na wawakilishi kutoka Chuo. Joyce alifana sana aiseee...(Dear Girlfriend wa sasa NASISITIZA ukiwa unasoma uzi huu uwe na utulivu) haha ha ha maana mnyonge mnyongeni haki yake apewe Joyce popote alipo.

Kwa huduma bora za Kariuki nilipona haraka na kurudi Chuoni na kuendelea na masomo na vipindi pia vya Luninga.

Kipekee namshukuru mno Msanii Roma Mkatoliki. He's a man and a half. Ni mtu wa watu. Amejaa Utu. Abarikiwe zaidi na zaidi.

Kuhusu rafiki yangu Nay wa Mitego kuwa sababu kuu ya kutokea hili, ingawa sijawahi kumwambia, niseme hana kosa, kila kitu Mungu anapanga na kwa sababu maalumu.

Shukrani sana Joyce, Hospitali ya Kairuki, IMTU, wanafunzi wenzangu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kugharamia matibabu yote.

Katika Mungu, imani zetu zijae. Tuwe wema kwa watu wote hujui siku wala saa utakapopata matatizo utasaidiwa na nani. Natanguliza Shukrani.

Suphian Juma,
Dodoma,
Septemba 14, 2021.

IMG_20210911_154515_109.jpg
 
View attachment 1936905
Kijana kule kwenye pori hakuna anayesogeleaga Ila sema walijua nyie ni wageni maeneo Yale mbona sisi tunafanya mazoezi pale karibu na geti Kuna uwanja na kule mbele kuna bar kibao za beach bubu na ganja kama kawaida na hakuna anayezingua maana tunaheshimiana anayevuta mibangi yake hasumbuliwi na hakuna wezi aisee labda walikuja watoto wa mtongani hao walishajua kuna college bash wageni wanakuja wakawakaribisha.
 
Kuna siku ilitokea ajali ya gari Cha kwanza nikauliza gari imeumia......

Niliisikia mama mzazi akinikemea alinambia uhai ni muhimu kuliko vitu....

Tangu hapo nilijifunza...

PEOPLE A TO BE LOVED & THINGS TO BE VALUED....

Pole Sana mkuu....stay blessed
 
Back
Top Bottom