Wasabato leteni ushahidi wa kimaandiko kuwa Mama Ellen G. White ni Nabii wa mwisho duniani

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
3,780
8,358
Wadau hamjamboni nyote?

Ndugu zangu Wasabato duniani mnaweza kutupa ushahidi au dalili kimaandiko kuthibitisha kuwa Mama Ellen G White ndiye Nabii wa mwisho duniani?

Je ni kweli kuwa baada ya Ellen G white hakutakuwa na manabii wengine na hata wakitokea watahesabika kuwa ni waongo?

Je ni kweli pazia la Unabii ulimwenguni limefungwa baada ya kuzaliwa na kisha kufa mama White ambaye kwenu ni Nabii?

Niwatakie siku njema


Matendo ya Mitume 2:17:

"Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto"
 
Ellen G. White alisisitiza kuwa yeye sio nabii licha ya waprotestant kumchukulia kama nabii.
 
Hadi useme methali hii ina maana gani?
Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.

Mithali 11:22
 
Back
Top Bottom