Kamuulize vizuri padre wako, anajua ukweli,anajua Hadi lini waliingiza fundisho la maria kupalizwa,wakaonelea wasingizie ufunuo 12 kwa kutumia Aya 2
Isome bila mihemko biblia utaielewa
Ufunuo 12:1
✓“Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.”
✓Mwanamke: katika unabii hutumika kuwakilisha “
#kanisa”, na kanisa la kweli linawakilishwa na mwanamke ambaye ni bibi arusi, ambaye ni bikira safi, na amevikwa jua, mwezi, na taji ya nyota kumi na mbili.
✓Wakati kanisa la uongo linawakilishwa na mwanamke ambaye ni kahaba na mwasherati.
¢Paulo anaandika: “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.” (2 Wakorinto 11:2).
Alikuwa akiwafundisha Injili ya kweli ili wasipokee uongo na kujichafua wenyewe, bali wakae katika kweli; maana kanisa ni msingi wa kweli (angalia 1 Timotheo 3:15), na hatimaye waweze kuwa kanisa la kweli ambalo ni bikira na liko safi bila doa wala waa lolote (Waefeso 5:27).
✓Katika Ufunuo 14:4 tunaambiwa kwamba: “Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake [makanisa], kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.” Sababu kwanini ni bikira na wasafi ni kwa kuwa waliifuata kweli ya Kristo wakatakasika (Yohana 17:17),
Pia walikataa kukubali mafundisho ya uongo yaliyotungwa na shetani katika makanisa makahaba yanayoungana na dunia ili kufanya uzinzi. Na siku ya kukamilika kwa ukombozi wote tunaona wanaitwa kama “mke wa Yesu” au “bibi arusi wa Yesu”, ikimaanisha kuwa walimtii Kristo na kukataa kufanya uasherati kwa kumtii shetani.
Maandiko yanapoelezea kanisa pekee la kweli ambalo wao peke yao ndiyo wataokolewa siku ya mwisho, siku zote yanalitaja kama mke wa Kristo;
Tunaona Ufunuo 19:7 inasema:“kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo [Yesu] imekuja, na mkewe amejiweka tayari.”
Hapa mke wa Mwana-Kondoo ni kanisa ambalo ni watu waaminifu peke yao, wanaomtii Kristo na wanawakilishwa kama Bikira safi kwa sababu hawakufanya uasherati kwa kumtii shetani na dhambi, wala hawakuamini uongo.
NI KWANI MUNGU ANALIITA/ ANALIFANANISHA KANISA LAKE NA MWANAMKE?
Sababu ya kwanini Mungu anapenda kutumia “mwanamke” ili kuwakilisha “kanisa” au “watu”
Ni kwa sababu mwanamke anapaswa kumtii mume wake na hapaswi kutoka nje na kufanya ukahaba na wanaume wengine;
✓hivyo hapa kuna aidha watu wawe ni watiifu kwa neno la Mungu ndipo wawe kanisa la Mungu, au wawe ni wakaidi wa neno la Mungu ndipo wawe kanisa la shetani;
✓ Na hivyo kumtii Mungu ndiyo ishara pekee inayowafanya watu kuwa kanisa au mwanamke safi na bikira anayetii neno la Mungu;
✓MAANA Paulo anasema: “Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. 24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.” (Waefeso 5:22-24).
✓Ni kwa utii pekee wa neno la Mungu ndipo watu wanaweza kujulikana kuwa sehemu ya mwanamke safi wa Mungu.
JE KUVALISHWA JUA KWA MWANAMKE KUNAMAANISHA NINI?
✓Jua: hapa limetumiwa kumwakilisha Kristo Mwenyewe; na kwa sababu mwanamke huyu au kanisa hili limevikwa jua; hii inamaanisha kanisa la kweli halijavaa mavazi yake lenyewe, bali limemvaa Kristo (Wagalatia 3:27) au limevikwa mavazi ya Kristo.
✓Mavazi hapa yanawakilisha “
#haki”, na hivyo kanisa hili kuvikwa mavazi ya Kristo inamaanisha kuvikwa haki ya Kristo; yaan, hawashindi dhambi kwa nguvu zao wenyewe, bali kwa neema ya Kristo pekee wanawezeshwa kuwa watiifu kikamilifu;
kwa maana imeandikwa: “Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki [Kristo] litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake [1]; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.” (Malaki 4:2).
✓Jua la haki hapa ni Kristo Mwenyewe, na mwanamke huyu kuvikwa jua haiwezi kuhusishwa na kitu kingine chochote katika Maandiko, isipokuwa ni kumvaa Kristo au kuvikwa haki ya Kristo.
✓Tukienda zaidi tunaona Maandiko yanahusisha kati ya amri za Mungu na haki yake. imethibitishwa na Mungu Mwenyewe katika Isaya 51:7 ambapo anasema: “Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu”. Haki yake inapatikana kwa kutunza sheria zake zote (angalia Wagalatia 3:10)