Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
WARAKA WA WAZI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DOKTA JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI NA WAZIRI WA TAMISEMI SULEMAN JAFFO JUU YA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA(CWT) KUKIUKA SHERIA ZA NCHI KWA KUSHIRIKIANA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NCHINI..
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daktari John Joseph Pombe Magufuli ninakusalimia sana, Shikamoo, pole na ujenzi wa Taifa .
Mheshimiwa waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo shikamoo, pole na hongera kwa ujenzi wa Taifa letu.
Mheshimiwa Rais, wewe ndiye waziri wa TAMISEMI na ofisi yako ina waziri anayeshughulikia TAMISEMI Suleiman Jaffo, hivyo naomba sana waraka huu uusome na kusaidia utatuzi wa matatizo makubwa yanayofanywa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa ushirika na wakurugenzi mbalimbali wa halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji kukiuka Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004,ukiukwaji WA Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,ukiukwaji wa Kanuni za Ajira za mwaka 2007 na 2017,ukiukwaji wa Tamko la Ulimwengu la Haki za Binadamu na pia ni ukiukwaji wa Agizo lako (Presidential decree) ulilotoa tarehe 01/05/2016 mjini Dodoma.
Mheshimiwa Rais Dk Magufuli, Lengo la waraka huu wa wazi kwako ni kuelezea mambo yafuatayo
(A) Uvunjaji wa sheria na Katiba unaofanywa na baadhi wasaidizi wako yaani wakurugenzi wa halmashauri kwa kushirikiana na CWT kuvunja haki za walimu wanyonge..
(B) Ufisadi mkubwa wa mali za CWT kutokana na Riporti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
(C) Uwepo wa Vyama vingi vya Wafanyakazi na Haki za Vyama hivyo mbele ya Sheria na Katiba ya Tanzania.
(UVUNJAJI WA KATIBA NA SHERIA UNAOFANYWA NA BAADHI YA WASAIDIZI WAKO YAANI WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KWA KUSHIRIKIANA NA CWT KUVUNJA HAKI ZA WALIMU WANYONGE.
Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, utakumbuka kwamba tarehe 01/05/2016 ukiwa mjini Dodoma uliagiza waajiri (wakurugenzi) wote nchini kuacha mara moja kulazimisha wafanyakazi wakiwepo walimu kujiunga au kuwaungwa katika vyama vya wafanyakazi bila ridhaa yao.
Mheshimiwa Rais, kwa kiasi kikubwa yaani kwa asilimia 98% ulimaanisha Wakurugenzi nchini waache mara moja kuwaunganisha walimu katika chama cha walimu Tanzania (CWT) kwa kuwa ndio chama pekee cha wafanyakazi Tanzania kinacholazimisha walimu kuwa wanachama wake bila ridhaa au matakwa yao.
Mheshimiwa Rais, naomba nikupongeze kwa kuliona hilo na kutoa agizo (presidential decree ) kwa waajiri na hilo agizo lako hakika ndio sheria inavyotaka pamoja na Katiba ya nchi. Kwa maneno rahisi ni kwamba, Agizo lako ndio takwa la sheria, katiba na matakwa ya walimu nchini. Kwa maana hiyo Heko Rais John Joseph Pombe Magufuli.
Mheshimiwa Rais Daktari Magufuli, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo uliapa kuilinda, kuihifadhi na kuitetea ibara ya 20(1) imetoa haki ya raia wakiwepo walimu kuchagua chama chochote cha siasa au kinachohusu maslahi mengineyo (kikiwepo cha wafanyakazi) kujiunga au kuanzisha. Aidha ibara ya 20(4) imekataza kulazimisha mtu kujiunga kwa shuruti chama chochote. Hii ina maana haki ya kukutana, kushirikiana na wengine yaani Right to association ni hiari na sio shuruti kama ambavyo Chama cha walimu na baadhi ya wakurugenzi wanavyofanya.
Mheshimiwa Rais Daktari Magufuli, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004 inakwenda sambamba na agizo lako kifungu cha 9 (1)(a) kinachotoa haki kwa mfanyakazi (akiwepo mwalimu) kujiunga au kuanzisha chama cha wafanyakazi kwa hiari bila shuruti. Kifungu hicho kimeeleza kwamba, mfanyakazi mwenyewe atajaza fomu maalumu itakayotolewa na chama cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria.
Kwa kuzingatia kifungu hicho cha 9 (1)(a) cha sheria, Serikali yako kupitia Tangazo la serikali namba 47 ilibadilisha fomu maalamu ya kujiunga na chama cha wafanyakazi kutoka kuitwa fomu TUF 6 na kuwa fomu namba TUF 15 ambayo fomu hiyo inatoa pia ruhusa ya mfanyakazi kwenda kwa mwajiri (mkurugenzi) kukata ada ya uanachama ya chama cha wafanyakazi.
Mheshimiwa Rais Magufuli, Chama cha walimu kwa kushirikiana na baadhi ya wakurugenzi wamekuwa wakiwakata walimu makato ya mishahara yao ya 2% kinyume na kifungu cha 61(1) kwani walimu hulazimishwa kukatwa fedha hizo bila kuwa wanachama wa CWT kwa kujaza fomu ya kisheria ya TUF 15 kama sheria inavyoagiza. Mheshimiwa Rais, kwa mujibu wa sheria hiyo hiyo ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004 kifungu cha 61(4) kimempa haki mfanyakazi kufuta ruhusa kwa mwajiri ya kukata makato ya uanachama kwa kutoa taarifa ya siku therathini (mwezi mmoja) kwa mwajiri na chama cha wafanyakazi.
Walimu wametumia kifungu hicho cha 61(4) kufuta ruhusa kwa waajiri ingawa hawakujaza fomu TUF 15 kwa kuwa wanalazimishwa kukatwa makato kinyume na sheria bado walimu wameendelea kukatwa na wakurugenzi kwa ushawishi wa CWT. Yaani wakurugenzi wanapewa ufafanuzi wa kisheria na viongozi wa CWT badala ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali au mahakama .
Mheshimiwa Rais Daktari Magufuli kifungu cha 61(4) kinasomeka hivi " An employee may revoke an authorisation by giving one month's written notice to the employer and trade union"
Kwa lugha ya kiswahili imeandikwa hivi " Mfanyakazi anaweza kufuta ruhusa kwa kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kwa mwajiri na chama cha wafanyakazi "
Mheshimiwa Rais Daktari Magufuli, CWT baada ya kuona walimu wameanza kujiondoa katika makato yao kwa kuwa ni kinyume na sheria katika baadhi ya mikoa na halmashauri , wametoa waraka wenye kumbukumbu namba AB.227/320/01A/116 ambao umejaa upotoshaji mkubwa wa kisheria na kwa bahati mbaya sana wakurugenzi wanaufuata waraka huo wa CWT badala ya kufuata ushauri wa kisheria kutoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali.
Walimu wameanza kujiondoa katika Chama cha Walimu (CWT) na kujiunga na vyama vingine vya wafanyakazi (Walimu) kama vile Chama cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) ambacho kilisajiliwa na msajili wa vyama vya wafanyakazi mwaka 2015 na kupewa namba ya makato ya kupokea michango ya wanachama namba 1234 CHAKAMWATA contribution. Changamoto wanayokumbana nayo Walimu hawa ni kukataliwa kuondolewa kwenye makato na waajiri kwa maelekezo ya CWT. Hapa kuna viashiria vingi vya ushawishi wa fedha yaani Rushwa kwani sheria iko wazi na katiba iko wazi kuhusu haki hiyo.
Mheshimiwa Rais Magufuli , naomba niwapongeze sana baadhi ya wakurugenzi au waajiri nchini ambao wamekubali kufuata sheria, kutii agizo lako la kisheria na katiba ya nchi kwa kuwaondoa Walimu katika makato ambayo yako kinyume na sheria. Wakurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa, Halmashauri ya wilaya ya Ileje, halmashauri ya wilaya ya Monduli, halmashauri ya wilaya ya Rorya, halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Temeke, Ubungo, halmashauri ya wilaya ya Mufindi, halmashauri ya wilaya ya Nyamagana na halmashauri nyingine nyingi .
Mheshimiwa Rais Magufuli, kwa kuzingatia kwamba wewe ndiye mwenye dhamana na TAMISEMI kupitia waziri Suleiman Jaffo na Katibu mkuu wake wa TAMISEMI ninaomba wakurugenzi wote nchini wapewe waraka kutoka ofisi yako ya Rais TAMISEMI kuacha mara moja kukata Walimu makato ya CWT bila ridhaa yako au kuwapa maelekezo kwa waraka waajiri wote kutoa ushirikiano kwa wafanyakazi kujiunga na vyama wavitakavyo kwa kuzingatia sheria kwa kujaza fomu TUF 15 ya kisheria.
Mheshimiwa Rais Magufuli, waraka huo ukitolewa, utakuwa umetetea Katiba ya nchi na sheria lakini pia utaondoa malalamiko ya uonevu na unyonyaji wa CWT ambao kwa miaka mingi wamekuwa wanyanyasaji wa walimu kwa kuwabagua, kuwanyanyapaa (hasa Walimu wa sekondari), kuwatenga na kutumia fedha zao kwa maslahi binafsi na kufuja mali hizo. Nina hakika Walimu wengi sana watafurahishwa na haki hiyo itakayotolewa kupitia waraka huo.
(B) UFISADI NDANI YA CWT NA UPUUZAJI WA WALIMU KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI.
Mheshimiwa Rais, Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa John Kijazi alimuomba mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kufanya ukaguzi kwenye chama cha Walimu (CWT) ambacho kwa kweli kwa miaka mingi sana kimekuwa kikidhihaki, kupuuza Walimu na watanzania kwa kutosoma mapato na matumizi ya chama wala kuwanufaisha Walimu kwa lolote. Hata wewe mheshimiwa Rais umekuwa shahidi na ulihoji katika mkutano mkuu wa CWT kuhusu usiri mkubwa wa CWT na kutonufaika kwa Walimu na chama hicho ambapo ulieleza wazi kwamba, ulipokuwa mwalimu wewe pamoja na mke wako (first lady) mlikatwa fedha na CWT lakini hamkuwahi hata kwa sekunde moja kuelezwa matumizi ya fedha hizo za Walimu .Ushuhuda wako huo ndio uhalisia mpaka sasa.
Mheshimiwa Rais, CAG amefanya ukaguzi CWT na kubaini matumizi mabaya ya fedha za Walimu wanyonge na ulaghai mkubwa wa CWT kuhusu wanachama.
CAG amejiridhisha kwamba pamoja na kwamba Katiba ya CWT inaeleza kwamba ina wanachama wa aina nne lakini chama hicho hakina idadi wala orodha ya wanachama wake. Yaani ni chama kinachokata Walimu makato lakini sio wanachama wake kwa kuwa hakuna ushahidi wa fomu za TUF 15 kiserikali kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya kujiunga na chama cha wafanyakazi . CWT wanajua kwamba, Walimu hawawezi kujaza fomu zao za TUF 15 kutokana na ubaguzi wao, usiri,ufisadi na uozo mwingine uliojaa katika chama hicho. Hivyo hutumia ushawishi mwingine kurubuni wakurugenzi kuanza kukata Walimu fedha bila walimu kuwa wanachama wao kinyume cha sheria.
Mheshimiwa Rais Magufuli, CWT wamejitapa kwamba wao wanawakata walimu wasio wanachama kwa kuzingatia kifungu cha 72 cha sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kwa Walimu wasio wanachama wa chama chochote cha wafanyakazi. CWT wanasahu kwamba duka la uwakala halipaswi kukatwa moja kwa moja kwenye mshahara wa mfanyakazi bali kutokana na ada ya uanachama kwa mujibu wa Kanuni za Jumla Za Ajira kanuni kifungu cha 37(1) na wanadai wanao wanachama wengi kuliko vyama vingine vya Walimu. CAG ameonesha kwamba CWT hawana orodha ya wanachama kwa mujibu wa sheria .
Mheshimiwa Rais, licha ya CAG kuonesha CWT hawana wanachama kwa mujibu wa sheria bali ujanjaujanja na ulaghai WA kuwakata Walimu na kujipa mamlaka ya kuwafanya ni wanachama wao, pia CAG ameibua Ufisadi mkubwa ndani ya CWT.
Mheshimiwa Rais Daktari Magufuli, CAG ameeleza kwamba kwenye CWT kuna matumizi ya shilingi Bilioni tatu, milioni miambili themanini na saba, laki Saba na elfu nane miatatu hamsini na nane (3,287,708,358/=) zililipwa bila kuidhinishwa na Katibu mkuu wa chama wala mweka hazina wa CWT na kuna viashiria vya ufisadi. Hii ndio CWT ya usiri mkubwa na kupuuza walimu tena bila wajibu wa kuwatetea walimu.
Mheshimiwa Rais, kama hiyo haitoshi, CAG amebainisha kwamba, ndani ya CWT hakuna nyaraka wala vielelezo vya matumizi ya Bilioni kumi na moja, milioni Mia tisa ishirini na nne, laki mbili na elfu hamsini na Mia sita ishirini na senti kumi na tatu (11,924,250,620.13/=).Fedha hizi ni nyingi sana na kitendo cha kutokuwepo kwa nyaraka za malipo ni kiashiria kwamba chama hiki cha CWT kimejaa ufisadi wa fedha huku walimu wakiendelea kuumia bila huruma.
Sambamba na hayo CAG amebainisha kwamba hata jengo la Mwalimu House si mali ya CWT bali ni mshirika kwa kuwa na hisa na taarifa za CAG zinaonesha jengo hilo limesajiliwa na BRELA kama Teachers Development namba 45719 na CWT haina maamuzi katika uendeshaji wake kwa kuwa ina share ndogo. Mbaya zaidi mapato ya jengo hilo hayaonekani na hivyo hakuna manufaa kwa walimu.
(C) VYAMA VINGI VYA WAFANYAKAZI(WALIMU) NA HAKI ZAKE MBELE YA KATIBA NA SHERIA
Mheshimiwa Rais Daktari Magufuli, Kwa kuwa CWT imeonekana wazi kukosa uadilifu, uwazi na usimamizi wa haki za walimu na kujaa ubaguzi, dharau, dhihaka na upuuzaji wa Walimu, Walimu wameamua kuanzisha vyama vingine vya walimu kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya nchi ibara ya 20(1)(4) na sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004 kifungu cha 9(1) na kifungu cha 10.Ninaomba kwa mara ya pili, ofisi yako iwaagize waajiri wote nchini kuheshimu uhuru wa walimu kuchagua vyama vya kujiunga badala ya kuwatisha, kuwalazimisha na kuwakataza. Ofisi yako itoe haki hii ya kisheria na kikatiba kwa walimu ambao wamechoshwa na CWT ambayo imeonesha kuwa ya hovyo na kandamizi.
Baadhi ya vyama vya wafanyakazi vilivyoundwa nje ya CWT ni pamoja na CHAKAMWATA na CHAKUHAWATA ambavyo vimesajiliwa na msajili wa vyama vya wafanyakazi na vinatetea walimu maeneo mbalimbali ya nchi kwa mujibu wa sheria za nchi.Vyama hivi vinakumbana na changamoto ya baadhi ya waajiri kukataa kuvitambua na kushirikiana navyo badala yake hufanya kazi kwa maelekezo ya CWT jambo ambalo ni kuumiza walimu, kupora uhuru wao wa kuchagua chama cha wafanyakazi na hivyo kupoteza morali ya kazi.
Naomba kuomba tena mheshimiwa Rais, ofisi yako ya Rais TAMISEMI iwaagize waajiri nchini kuacha kufuata maelekezo YA CWT bali maelekezo ya sheria, katiba, mikataba ya ajira,Tamko la Haki za Binadamu Ulimwenguni pamoja na matakwa ya Walimu na msaada au ufafanuzi wa kisheria waajiri wapate kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG) au Mahakama ya Kuu kitengo cha Kazi na sio kupata ufafanuzi wa kisheria kutoka Katibu mkuu CWT ambaye Kwanza ana maslahi na ufafanuzi huo na mbaya zaidi ufafanuzi wake umejaa upotoshaji mkubwa.
Naomba kuwasilisha
..........................................................
Daniel Ezekiel
Mwalimu
danielezekiel2222@gmail.com