Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,083
Huu mwezi kumetokea matukio mengi kwa Walimu na wanafunzi, Walimu wakitoa vipigo vikali sana kwa wanafunzi, wanafunzi wakipokea ngumi chembe kidevu, ngumi za macho, fimbo 50.
Sikatai wanafunzi wasipigwe lakini, piga fimbo zako tatu au nne then pita kushoto, sasahivi mitandao imeleta mapinduzi sana, mfano leo mtoto kutoka kasulu kapigwa na Mwalimu leo asubuhi, mchana video imesambaa, namaanisha nini?
Zamani hata sisi tulipigwa, fimbo nyingi mno lakini hata tukienda kusema nyumbani wazazi hawakua upande wetu, walikua wana waheshimu walimu na kuona maamuzi anayoyafanya ni sahii. Pia mitandao ilikua haipo, kwa hiyo hata ukipigwa ukavuja damu akija mzazi yanaisha ofisini, sasa hivi mpaka uko kasulu watu wanamiliki simu.
Maadili yamepungua mzazi yuko upande wa mtoto, kwa hiyo mtoto hata azingue vipi mzazi wala haweki mazingira ya kumkanya mwanae sasa Mwalimu ni nani umbadilishe mtoto tabia wakati mzazi wake ameshindwa?
Mwalimu nenda shule mapema, fundisha darasani anaelewa nenda naye asieelewa, mtukutu achana naye, saa 4 mapumziko toka nje ya shule kavute fegiii saa 7 unarudi unazuga zuga, saa nane unaenda kwenye mitikasi yako, Mwisho wa mwezi chukua chako kale na mke wako.
Ila ukijifanya unajua kunyoosha tabia kwa kizazi hiki?, believe me utaishia kwenda jela, hakuna Mwalimu anaempiga mtoto bila kosa, lakini siku ukimpiga mtoto ukapelekwa jela huyo mkurugenzi unaempambania shule yake ifanye vizuri ndio atakua wa Kwanza kukuandikia barua ya kukufuta kazi, ili uadhibiwe bila kinga ya mtumishi wa umma.
Ninajua shule za kata,bila fimbo hutopata division 1 au 2, lakini weka document zako zikae vizuri, lesson plan, scheme of work, lesson notes, hata wakifeli wakija kukukagua unakua na supporting document.....
Kubwa zaidi, jishughulisheni wekezeni, nyie sio wanyonge kihivyo, ni basi tu kazi haina posho lakini kwa level yako ya elimu iwe degree au diploma, unawazidi mshahara wafanyakazi wengi wa Halmashauri. Mwalimu wa sciences mwenye degree anamzidi Mhasibu,afisa ugavi, afisa maendeleo n.k, kwa hiyo tujitafutie posho kwa kufungua duka na kujikita kwenye ujasiriamali.