Wapinzani wa Dr Magufuli waanza Kujitokeza

ANKOJEI

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
996
743
Takribani miezi kadhaa baada ya Magufuli kushinda uchaguzi kwa matokea ambayo yalitegemewa kugomewa na vyama vya upinzani endapo mshindi yeyote wa CCM angeshinda, SASA wapinzani wake ambao si wa kisiasa bali wa kisera na kiuchumi wameanza kujitokeza.
Baada ya siku 60 za kuchaguliwa kwake wapinzani wengi walikaa kimya hasa kusubiria uchaguzi wa baraza la mawaziri lakini Magufuli aliwapiga chenga na kuendelea kupiga kazi Muhimbili, Bandarini na TRA pamoja na TRL. Wengi hawakujua nini hasa mbinu za Magufuli katika kuhakikisha anatimiza ahadi zake.
Siku za hivi karibuni yameibuka maswali mengi lakini makubwa ni:

1. Je Magufuli ana mbinu na uwezo wa KUKUZA UCHUMI (ECONOMIC GROWTH STRATEGY)
2. Je kubana kabisa na kufuata sheria za kodi 100% ni njia sahihi na ya Kudumu? (SUSTAINABLE)
3. Je mfumo wa serikali na chama cha CCM uliotufikisha hapa utaweza tena kwenda na (COMPATIBILITY)


Ndipo nikalazamika Kuangalia Clinton alifanya nini?
Clintoni aliingia Madarakani na kukuta Uchumi wa Marekani ulio mbovu kabisa, nini alikifanya?

1. Kusimamia mapato na matumizi ya serikali na hivyo kufuta nakisi ya bajeti na kuhakikisha serikali inajitegemea kibajeti bila kukopa kopa ovyo.
2. Hivyo serikali ilipata pesa ya kulipa deni la Taifa lililokuwa kubwa
3. Kuunda sheria ya kazi na ujira kwa wasio na kazi pia wasiojiweza na waleao watoto katika mazingira magumu
4. Kupunguza riba za mikopo
5. Kuweka ukomo wa mfumuko wa bei
6. Kufungua milango ya uwekezaji toka nje ya nchi
6. Kuwekeza katika mtaji wa watu, elimu na ufundi pamoja na utafiti
7. Kulipisha kodi kubwa kwa matajiri na kupunguza kwa maskini

Matokeo yake uchumi wa Marekani ulifurika haraka sana
1. Deni la taifa lilipungua
2. Uchumi ulianza kukua tena
3. Ajira zikawepo
4. Wagunduzi na watafiti wakaongezeka

Nashawishika mambo Mengi aliyoyafanya Clinton yanashabiana na Magufuli ndio mana nasema ni Clinton mpya wa Africa.

Sasa tukirudi katika maswali haya matatu,
1. Je anao uwezo wa KUKUZA UCHUMI (ECONOMIC GROWTH STRATEGY)
2. Je kubana kabisa na kufuata sheria za kodi 100% ni njia sahihi na ya Kudumu? (SASTAINABLE)
3. Je mfumo wa serikali na chama cha CCM uliotufikisha hapa utaweza tena kwenda na KASI HII YA MAGUFULI

Wataalamu wanasema ili nchi za Africa zipate kuondokana na Umaskini basi uchumi wake lazima ukue katika kiwango cha zaidi ya asilimia 10 yaani double digit growth. Kama Magufuli hataifumua mifumo inayozuia ukuaji wa uchumi kwa kasi pamoja na kukibana chama chake basi huenda tukabakia na uchumi wa chini ya 10%. Pia kuna uharaka wa dola kufikia 1800 na baada ya hapo iendelee kushuka ili wanachi wafurahie ukuaji wa uchumi wao.

Ingawa wapinzani hawa wameanza mapema kupiga za chinichini mimi binafsi nawaunga mkono lakini napendekeza kuwe na midahalo ya wazi kumshauri rais nini afanye ili kukuza uchumi wetu. Atahitaji pia kuwa na washauri wa kiuchumi imara ambao si wanasiasa.

Kama wewe ni mjasiriamali basi unaweza kuchungulia sekta kadhaa zinazoonyesha matarajio ya kukua kwa haraka sana ndani ya miaka 5 ya utawala wa magufui hapa chini.....

Price Watch Afrique: MAGUFULIFICATION: CLINTON MPYA AFRICA

Na pia ukitaka kujua nini Magufuli amekifanya ndani ya siku 60 za utawala wake bofya hapa

Price Watch Afrique: SIKU 60 ZA UTAWALA WA MAGUFULI

Swali linabakia "ATAKUZA UCHUMI?
 
Kuna vitu usipocheza navyo umasikini siyo wadudu au wanyama useme ni utaviua uishe bali umasikini ni ugonjwa ambao vimelea vyake havionekani ata kwa darubini...! Hivyo ata kuuondoa hatuitaji nguvu zaidi ya akili..! Moja huwezi kuwekeza pesa nyingi kwenye elimu afu watu unao zalisha manpower haitumiki hesabu how many graduates wako mitaani.

Kwa rais mjinga ataona shauri yao km hawataki kujiajili anasahau anawadai millions of money.

Pia uwezi kuongelea maendeleo bila kuongelea technology hapo tutaumbuka tu na jitihada zote hatutakwenda popote!

Matumizi sahahihi ya rasimali za nchi, ardhi, maji, madini na gesi, mistu na wanyama vinatumikaje ni swali gumu asiloweza jibu magufuri.

Magufuri mnao muona atafanya kitu ni wale mnaomlinganisha na kikwete na hamna mizania ya maendeleo hivyo mnakosa vipimo sahihi vya maendeleo.

Elimu hamna sehemu ya kupima ili kujua km ni bora au la..! Binafsi kufa au kudumaa kwa technology kwa miaka 50 ni kipimo tosha kuwa elimu tuapatayo licha ya kuwa ni kwa watu wachache bado ni fake..

Naomba kuishia hapa.
 
Endeleeeni kumsifia mgema! Kila siku habari ni zile zile! Lakini huku Uswahilini Unga haujashuka bei,sukari haijashuka,ngano ndo usiseme! Kiujumla hata mfukuzana kazi vipi,sisi huku maisha yetu hayabadiriki! LASTLY UMETUMIA WRONG RELATIONSHIP KWENYE ARGUMENTS ZAKO,wakati US wapo kwenye Economic Development,sisi tupo kwenye Economic growth! So kuilinganisha US na Tz ni sawa na ushuzi na marashi
 
Lyatonga Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alifanya mengi ya kusifiwa na alipendwa Sana kama JPM,lakinii Kuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kumkabidhi aendeshe uchumi wa nchi
JPM = ALM time will tell
Both, Ni wajuzi WA kila kitu,si wakushauriwa na yeyote
 
Siasa za vyama vingi zina lengo zuri, popote pale zinaposimamiwa kisayansi. Tatizo la aina hii ya siasa haswa barani mwetu afrika, ni ule uduni wa elimu wa wahusika wakuu wa siasa hizi.Tumegeuza uchambuzi wa hoja kuwa sababau ya kumtusi mtoa hoja, tumeshindwa kuitambua maana ya vyama vingi. Wapinzani wa magufuli wanaweza kuwemo hata ndani ya familia yake. Kilicho muhimu ni kujenga hoja mbadala zenye mantiki, busara na cha muhimu zitoke ndani kabisa ya moyo wa yule anayezitamka. Naamini tunaweza kuongozwa na mfumo wa vyama vingi na bado tukazikana, tukasaidiana kiuchumi, na kilicho muhimu kabisa, tukapendana kama Watanzania.
 
mimi naona hapa dunia anae weza ni wewe peke yako!! mtu hujui kuwa Rais tunaanza na herufi kubwa hata lingekua katikati ya sentensi ndio uweze kusimamia uchumi au kumkosoa Magufuli ambae Dunia nzima wamempa credit kwa namna alivyo endesha serikali kwa muda wa siku 60 tu.
 
 
Huo uwezo atautoa wapi? Nani alikwambia huyo jamaa anashaurika? Sasa hivi MAHAKAMA ya ARDHI imezuia mwendelezo wa bomoa bomoa lakini sitashangaa kusikia kuwa Magufuli ameagiza bomoa bomoa iendelee! Na alaaniwe aliyechakachua matokeo ya jinsi wananchi walivyokuwa wameamua! Sisiem haina uwezo wa kukuza uchumi. Siku wakifika tarakimu 2 za ukuaji uchumi mniamshe hata kama nitakuwa nimelala!
 
" napendekeza kuwe na midahalo ya wazi kumshauri rais nini afanye ili kukuza uchumi wetu."

Clinton wa Marekani aliendesha nchi kwa midahalo ili na wetu aige!
hii midahalo ya vijiwe vya kahawa vimetusumbua utawala uliopita, kila kukicha linaanza jambo jipya kabla la awali halijatekelezwa, mf sekta ya elimu.
 
Unaonekana una wivu..
 
I humbly think kuna vitu vya msingi sana serikali ya awamu ya 5 inachemka.

Kimoja ni utawala wa sheria na kanuni. Tumerudi nyuma kwenye hili kwa pretext ya ku-clean up the mess. Well JK alipokosea sio kufuata utawala bora, I think he ranked very highly kwenye kuachia uhuru wa vyombo vya sheria, na ilikuwa sehemu aliyolaumiwa zaidi. kwani ilionekana hana maamuzi,wakati kiuhalisia aliachia uhuru kwa vyombo kujiendesha kwa kufuata mipaka yao, Kilichokosekana ni proper enforcement, na kilichoharibu ni abuse. sasa huyu jamaa amesoma tofauti kabisa, ndio wazungu husema if it's not broken, do not fix it. Tutarudi nyuma kwenye hiki kipengele sana tu. kwa sababu kiongozi aliyekuwepo hajui mbinu za ku-enforce utawala bora na kuzuia abuse. Blanket decrees is not what a democratic Tanzania wants it's what communist CHINA or North Korea might want.

Swala la pili, so far tune ya Magufuli ni "austerity". Shida ya austerity ni kuwa haikuzi uchumi. hivyo ndoto za double digit growth tutazisikia kwenye bomba. Bahati mbaya hakuna mwekezaji anayependa red tapes, huu ni ukweli mchungu. hatuwezi kuvutia wawekezaji, na kuwawekea sheria ngumu kama za jela at the same time. nchi nyingi zinazofanikiwa kukuza uchumi wakati wa "austerity" japo kidogo ni zile zenye internal capacity, je TUNAYO? Kama hatuna basi tujiandae kuwa na special economic zones zitakazovutia wawekezaji wawekeze bila kulipa kodi kubwa. tusijidanganye kuwa kila mfanyabiashara lazima alipe kodi, na kuwa kukusanya kodi kubwa ndio maendeleo ya upesi. Si kweli, huwezi kukusanya kodi kubwa wakati hakuna biashara za kukusanya hizo kodi. Ni ujinga mkuu. Hata hao china tunaojidai kuwakopi na kuwasifia walianzisha Shanghai,Tianjin, Shenzen special economic cities, which were dirt cheap to do business in so as to attract investments. This was 40 years ago. Today Shanghai, Shenzen and Tianjin are among China's biggest cities and the ones with the highest incomes. Moral of the story is Investments do not go where there are high taxes and endless red-tapes., it's the opposite. Je kama taifa kwa wakati huu tunataka kodi kiasi au ajira nyingi? Ikulu hili jibu ama halipo bado, au wanaogopa kulitaja, tusidanganyane wanataka vyote. You can't have your cake and eat it.

Swala la tatu ni Upimaji wa matokeo, wataalamu huita ME. Huwezi kuanzisha kitu kipya bila kuweka njia utakayopima kupima ufanisi. Na hili limekuwa kosa la magufuli toka akiwa waziri. The guy is obsessed with Quantity not Quality. Hivyo tutegemee utitiri wa decrees, utitiri wa vitu vipya visivyozingatia Quality. Kama unabisha katazame kilomita za barabara zilizojengwa na Mh,halafu fanya uwiano wa Quantity na Quality. That is what we should expect for the next 10 years.

Swala la nne ni kutokuambilika. Sasa hivi huko maofisini ni mwendo wa AMRI tu, watumishi wa serikali wamekuwa kama ma-zombie, Bosi akipewa amri ni kutetemeka tu, anachofanya ni kuishusha chini kama ilivyo, hachekechi. Wanaopokea amri nao wanatekeleza kama hawana ubongo. So far ni kuomba mungu hizi Amri ziwe sahihi na zisizo na makosa ya wazi, kinyume na hapo tutegemee kuwepo kwa beurocratic blunder za kutosha awamu hii. Kwa mfano halisi wa hili tazama structure ya baraza la mawaziri. Kuna kuboronga kwingi, ila nina uhakika hata Balozi Ombeni hana guts za kumwambia bosi wake hapa tumechemka, na the fact kuwa kajaza faculty kwenye wizara nyingi, inamaanisha hakutakuwa na ushauri kutoka chini kwenda juu, kwani ma-prof wetu wa nchi masikini tunawajua hulka zao. wao ndio alfa na omega wa kila kitu, ndio maana unakuta prof wa kilimo yuko bize kuchambua uchumi kwa mwamvuli wa uprof wake, wakati hajui kuwa ufahamu wake huko unaweza kuwa sawa na first year wa uchumi chuoni. In 10 years time people might remember JPM as Bwana haambiliki.


Kwa kuhitimisha, bado ni mapema kujua with certainty direction ya serikali ya Magufuli, ila nikimtazama Magufuli, na Majaliwa sioni vibrancy inayohitajika kwa 21st century modern leaders. I expected this to be corrected by during minister of finance appointment, but that was not the case. Kuna kujidanganya flani hivi kunaendelea miongoni mwetu kuwa kuna mabilioni ya mapato ambayo yakidhibitiwa vizuri Tanzania itakuwa nchi ya asali na maziwa. Si kweli, Tulishapitia hiki kipindi cha kudhibiti kila kitu, na tulikuwa na kiongozi (Nyerere) mwenye uelewa mpana mara 100 ya huyu wa sasa lakini kutokuambilika kwake kukawa downfall yake. JPM asijidanganye kujifungia TZ, ku-crack down on each and every cent kutaleta neema, Tanzania haina uchumi wa kiwango hicho, hata ukikusanya kila shilingi iliyoko TZ ukapeleka Hazina bado sisi ni nchi maskini. we need more, sio amri pekee.

Ni muhimu zaidi Magufuli akawaambia watanzania ni vitu gani atafanya kwa kiwango gani. Kama ni uchumi atoe projections, kama ni elimu atoe figures, ili tuweze kumpima, biashara za kusema nitaboresha, nitakomesha, nitasimamia ni too vague. hazina mantiki ya kisomi. Hata JK alisema ataleta ajira,n.k kwa kuwa hakuulizwa ajira za aina gani, ajira ngapi n.k, mwisho wa siku akaja kuhesabu hata waendesha bodaboda na wamachinga.
 
 
Uchambuzi mzuri na wa kujenga sana. Thanx nimepata somo..
 
I reserve this article for further reference!
 
Hakika hawezi kuza uchumi maana akili zao ndogo zile zile, watu wale wale hamna jipya katika serikali ya ccm
 
Waliowengi wanaomba Magufuli ashindwe ili wafaidike Kisiasa, hivyo inawezekana hata wanaomshauri miongoni mwao ni wale wanaotaka afail.
Hao hapo chini wanapiga maombi Magufuli ashindwe na alegee kabisa.
 
ANA MFUMO WA KIIMLA KAMA SADAM WA KUWAIT AAA WA LIBYA..
-KHAHAHAAA.....NDIYO MAANA NAJUTA KUMPA KURA YANGU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…