Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,609
Sakata la kugenisha bandari na rasilimali za Tz-bara Wapinzani siyo silaha sahihi kushinda vita.
1. Ni ukweli usiokanushika kwa ushahidi wowote ule kwamba Wazungu ni watu wasioitakia mema Afrika. Watu kama Tundu Lissu na Lema siyo wa kutegemewa kusaidia kushinda vita hii kwa sababu wataishia njiani vita ikingali mbichi. Hii ni kwa sababu watakuwa wanatetea jambo ambalo wazungu wanalitamani siku zote kuona linatimia (unyang'anyi) kwa njia ya ugenishaji.
Asili ya mikataba mibovu ilianza 1884-1885 na Wazungu hao hao ambao leo ndiyo wafadhili na walinzi wa Lissu na Lema. "Siku zote akulindaye huwezi kumuhujumu" hivyo Lissu na Lema naona mbeleni wanaenda kuungana na serikali, Bunge na NEC-CCM kutetea DP World ili nao wazungu waendelee kuwapa shavu (support) ambayo Tz na Chadema haviwezi kuwapa.
2. Wapinzani hawa hawa wamezoeleka sana majukwaani na masikioni mwa umma kwa kutofanikisha chagizo za nchi wanazozitumia kutengeneza agenda ya taifa, hivyo mpauko wao unatafsiriwa na usemi huu (Sheikh wa zamani ndani ya kanzu mpya).
3. Wapinzani kwenye agenda hii watataka kujitengenezea Party Supremacy ili kuwagawa kama ilivyokuwa kwenye mchakato wa Katiba Mpya "Utengano ni udhaifu"
4. Viongozi walewale wa upinzani siku zote, CCM inawajuwa hadi kwa vinasaba vyao na bei zao. Tutarajie matokeo gani?
5. Wameishaanza kuipunguzia kasi ya moto agenda hii ya kupinga ugenishaji wa rasilimali za taifa; kwa kupenyeza agenda ambayo tayari imebeba roho wa ufu ya Katiba Mpya "mvua za masika na za vuli haziwezi kunyesha kwa pamoja kwa wakati mmoja" "kila jambo na muda wake" "huwezi kuchanganya samaki na nyama kwenye chungu kimoja"
6. Hii agenda inahitaji umakini wa ziada maana tazama imeishagawa wanasiasa, media, viongozi wa dini, wanaharakati, viongozi wastaafu, mawakili nk.
Live it or leave it.