Wapinzani hawajashindwa kuing'oa CCM, tatizo ni mfumo

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Tukiwa tu wakweli na tukaacha unafki na ukweli utatuweka huru daima, kwa wanaofikiri kua wapinzani wameshindwa kuitoa CCM madarakani ni uwezo mdogo sana wa kufikiri pasina kuzingatia reality.


KUMBUKUMBU YA UCHAGUZI 2015,

Nakumbuka sana jinsi Polisi hawa. walivyowakamata sana wagombea wa upinzani wa nafasi mbalimbali wakiwatuhumu kua kwa kufanya fujo,lakini ukitazama upande wa pili hakuna aliyekamatwa na polisi wala kuzuiwa kufanya fujo, tena mifano ni mingi tu.

Wasimamizi wa majimbo ya uchaguzi ambao ndio wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na makada wa CCM ndio waliokua wakichelewesha matokeo kwa makusudi pindi anaposhinda mpinzani, hili tatizo lilikuwepo kila mahali.


Wakati January makamba akitoa mrejesho wa uchaguzi upande wa CCM, kule vijana waliokua wakitoa matokea ya wagombea wa UKAWA wakakamatwa na polisi, eti kuna watu wananyanyua midomo wapinzani hawawezi kuing'oa CCM.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI,


Wakati wa uchaguzi mkuu 2015, Jaji Damian Lubuva alikua mwenyekiti wa tume, Kailima Ramadhani ni mkurugenzi wa tume na wote ni makada wa CCM wateule wa mwenyekiti wa CCM mtegemee kuwe na fair play kweli?

Yani Match commissioner wa mchezo kati ya yanga na simba atoke yanga,waamuzi wote watoke Yanga,maandalizi yote ya mchezo yafanywe na wanayanga mtegemee Simba washinde kweli? Kwa usawa huo simba wasilalamike waonekane wakorofi.


Kwa watu wenye uwezo Mdogo wa kufikiri muache kumwandama Lowasa kua alishindwa, hamjui nini kilichokua nyuma ya pazia mkae tu kimya.Jioneeni aubu kulizungumzia hilo juu ya ukweli uliodhahiri.
 
kama aliamuwa kukaa kimya ili maisha yaende,
.Acha nasie tukae kimya ,maana kutolewa kucha kwa plaiz nako mmmh

 
Wapinzani hawajawi kushindana na CCM tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Hushindana na dola ( polisi, usalama, jeshi, mahakama, Tamisemi na Tume ya uchaguzi).
CCM huingia madarakani baada ya dola kumaliza mchuano na wapinzani.
 
..tuache kulalamika.

..wananchi walikuwa tayari kuchagua ukawa, ila Edward Lowassa alikuwa anakatisha tamaa.

..Ukawa wangeweka mgombea Uraisi mwenye ushawishi, na machachari mwenye uwezo ws kujibu mapigo ya ccm, naamini wananchi wangewachagua.


..kwa maoni yangu, Ukawa walikuwa na kura nyingi(ushawishi mkubwa) zaidi ya ccm wakati kampeni zinaanza. Lakini kura hizo zilikuwa zikipungua kadiri kampeni zilivyokuwa zikiendelea.

..makosa yaliyofanyika 2015 yasirudiwe tena. Kuna kura za kutosha kuweka Raisi na wabunge toka Ukawa kinachotakiwa kufanyika ni kuwapa wananchi wagombea wazuri.



cc Nguruvi3
 
Mkuu kuna factors mbili, ''internal and external''

External: Ni kweli kuwa wakurugenzi wanaochaguliwa na mwenyekiti CCM hawaweza kutenda haki. Tuliona hili pale jina la mtu lilipoondolewa na kisha kurudishwa

Tume ya uchaguzi: Hili tumeliongelea sana. Tunakumbuka Lubuva alivyoyumbishwa kila mara, leo tutatumia vifaa vya kisasa, kesho hili keshokutwa lile
Ukitazama, tume ilikuwa inafanyia kazi maagizo ya serikali ya CCM

Wajumbe wa tume kubadilishwa siku za mwisho wa uchaguzi kwasababu Rais(mwenyekiti wa CCM) ana mamlaka hayo.

Wajumbe hao sasa wana nyadhifa nyeti. Inaeleza kitu

Polisi na vyombo vya dola kutosimamia haki, hilo halina mjadala

Internal
CDM hawakuwa na mgombea mwenye ushawishi.
Dr na Mbowe wameongoza 'failures' za kutosha ni unlikely wangekuja na kitu tofauti

Focus ya CDM ilikuwa kupata abunge wengi na pengine kudhibiti 2/3. Ingewezekana

Kubadili mgombe dakika za mwisho ilileta sintofahamu miongoni mwa wapiga kura.
Na kwa bahati mbaya mgombea hakuwa na muda wa kujieleza

Tumaini la wabunge kwa jitihada likafa ikitumainiwa mgombea angekuja na wenyeviti20. Hawakuja na waliokuja hawakuwa na impact

Kwa hilo wakapoteza focus ya Bunge na kujikita kwa mgombea waliyetegemea

Mgombe aliyekuja hakuwa na ushawishi. Kuzindua kampeni ilikuwa failure ya kiwango cha juu. Watu walitegemea mafuriko zaidi ya message. Hakukuwa na message yoyote

Pamoja na kutokuwa na message mgombea hakuwa tayari kujisafisha

Ilikuwa mikutano ya dakika 5 ikitegemewa wingi wa wahudhuriaji ungetosha.
Wahudhuriaji waliondoa bila message na hilo liliawaathiri sana

Ukichanganya factors zote utaona kwanini walishindwa.

Moja za nje ambazo hawakuzizuia tangu awali. Huwezi kwenda uchaguzi ukijua ni unfair

Pili, kwa kutumia nguvu ya umma, hakukuwa na ushawishi kutoka kwa mgombea

Tatu, focus ya jitihada ikaondoka na kutegemea majaliwa ya mgombea

Suala ni kuhakikisha walioongoza 'failures' za siku za nyuma wanakaa pembeni.

Hapa nina maana Mwenyekiti wa CDM na timu yake

Halafu timu mpya ndiyo itaangalia nini cha kufanya mbele ya safari
 
kama aliamuwa kukaa kimya ili maisha yaende,
.Acha nasie tukae kimya ,maana kutolewa kucha kwa plaiz nako mmmh

Mkuu unawadanganya wapinzani. Si mfumo ni wao hawako makini na hata hivyo ukanda umewatawala. Kosa walilofanya ni kumuacha Slaa aondoke. Huyo ndiyo angeipotezea usingizi CCM. The Man is so smart and hana doa. Hawa waliopo wote majizi mwanzo mwisho. Usidhani watanzania ni mbumbumbu. Humu wanawakuza vichwa mbaya but wanawajua fika. Yaani Mbowe au Lowa awe Rais wa nchi hii kweli???!!!! Nooooooooooll!
 
Tatizo ni lao hawaandai viongozi. tatizo lao kuokota viongozi.wanao toka ccm.maana .wanapiga kelele.hawa mafisadi wakubwa.baadae.wanasema .oohuyu mzuri.anafaa sana .wana sahau wao wali mchufua.1 waangalie njinsi yakupata viongozi bora na si bora viongozi.wakuteuliwa na kiongozi..mmoja.2wakumbuke walio yasema nyuma..3waache ukanda ktk maswuala ya uongozi wajuu.has a ngazi zakugombea urais.3wajenge chama .kwa hoja nasera za chama nasio.kutumia matukio .kua ndio ajenda kuu,4 kueneza Sera zao kila kona ya inchi na nini msingi ya Sera kwa uma .5mtu yeyote mwenye kashifa asitumike .kwa shuhuli yeyote ya chama ili watu wasiwe nama swali yakuuliza.6kubadili kiozi has a mwekiti .maana kila viongozi ananyota yake.7wasi tegemee .mitandao.yakijamii.kwa kampeni yamatukio ili wakubalike.hilo nikosa kubwa .itumike kueneza Sera za chama ili watu wengi wawaelewe .maana uchaguzi ukianza .wenzao watasema .tuluahidi .maji na umeme vijijini .afya .elimu .utitiri wakodi.watumishi hewa .mafisadi.rushwa.mabarabara. Nk.kama hawa watu wametekeleza.yote au baazi yapi kwenye mikakati.nawali wa hahidi hivyo.barabara za juu .vivuko.meli..ndege .watashinda tu uchaguzi..nyie mbali na ho Roma katekwa .Mara hili.ku shika dola ningumu.
 
Watanzania wa sasa ni waerevu mno. Huwezi kuwa na ubongo mdogo halafu ukajiona una akili katika jukwaa kubwa kama hili
 
Mkuu joka,
Kama wapinzani tunaotaka waitoe ccm ndio hawa aina ya kina sumaye, afadhali hiyo tume iendelee kuwabeba ccm.

Can you imagine, mtu aliyehamasisha uhalifu kwa kuwahakikishia wahalifu kwamba hawataguswa ili mradi waisaidie ccm (tundika bendera ya chama) eti leo ndiye masiha?! Disgusting.
 

..huyu anayewaambia wananchi "MWAFAA " nadhani ni mbaya zaidi.
 
Tena hata nape amesaidia sana kuuweka wazi zaidi ukweli huu ,
akidai alikaa porini miezi kadhaa na ameirudisha serikali ya ccm madarakani !
Moja, kunakura za ccm tulizo ona zikipigwa kabla ya Siku yakupiga kura./uchaguzi.
Pili,kuna malori,bodaboda na magadi madogo,yalikua yakisafirisha kura zilizowekewa vema kwe picha ya magufuli.
Hivyo basi,kwakua nape alikua porini ili ccm irudi madarakani,inamaana walishajua ushindi niwa Lowasa,kwakua hakuna mwenye kuipenda tena ccm.
Ushahidi wa hili ni Yale magari ya polisi yaliyonunuliwa kwa ajili ya uchaguzi na zombie kupelekwa Zanzibar.
Hivyo ni hakika kabisa bila shaka yoyote,baada yakugundulika kwe mitandao wakipiga kura katika vyumba,wakahamia porini na nape ili kazi hiyo iwe rahisi,wakilindwa nakuifanya kwa nafasi zaidi.Njombe wananchi,walizuia gari lililokua na kura za ccm wakasambazwa na policcm
Kama niuongo nape akanushe,wakati wa uchaguzi alikua anafanya nini porini ?mafunzo ya mgambo,uchawi !,nakwanini mpaka akaeporini,ili kuirudisha ccm madarakani ?na akatangaza goli la mkono kwa uhakika akiwa kifua mbele akijua kura zinapigwa porini.hivyo kuweweseka kwa nape ni haki yake,na ni malipo yakudhulumu ushindi wa waliowengi,kwa manufaa ya wachache (ccm),tena wakitumia askari tunaowalipa kwa kodi zetu.
Nape kwa hili hata wa mama wote wa mtama,wakamue maziwa ili nape ajisafishe, hata takata licha ya kuwakanyaka makalio yao ! Muda ni mwalimu,nape ataongea mpaka siri ya kuiba kura za Lowsa,kama hawatamteka,tusubirini.
 

Lowassa na chadema walilijua hili kabla ya uchaguzi?? au ndio unawaambia wewe leo??

halafu walitegemea nini ? kushinda mbele ya wana CCM hao??

yaani umemfanya lowassa kama katoto sasa! unakatetea!

sioni sababu ya kwenda kwenye uchaguzi na tume hii ya uchaguzi!!
 
Kwa hiyo ccm ndio wanaandaa wagombea, ila kama huyu naye kaandaliwa basi ipo kazi.
 
Kuwaambia wafyaa huku anakemea rushwa ufisadi na kuijenga ni bora kuliko asiyesema lkn hana uwezo

..huyu aliyeuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa mnaamini ni msafi? Akanunua na meli mkweche akidai ni mpya. Sasa hivi ukihoji kuhusu meli ile unaweza kushtakiwa.
 
Ni kweli tatizo ni mfumo wa ubabaishaji wa Wapinzani ndio maana hawachukui dola. Kweli kabisa
 
Hakuna popote duniani ukute mshinda atengeneze mfumo wa kushindwa. Kila kitu kinaenda kwa sheria, sheria hupitishwa na bunge kwa kupigiwa kura na walio wengi hushinda. Hakuna nchi yoyote duniani inayoamini upigaji wa kura ukute eti wenye kura chache washinde.

Kwenye Bunge la Katiba, ni wazi tangu siku nyingi CUF wanataka serkali mbili baadaye Muungano ufe tuwe na Serkali ya Mkataba.

CHADEMA wakaona nafasi nzuri ya kutawala wakajaza watu wao kwenye Tume, wakaja na hoja ya serkali tatu iwe rahisi kugawana, CUF kule na wao huku.

Lakini ni jambo la msingi la tangu zamani na ndiyo maana damu ilimwagika Zanzibar, haiwezekani hoja ipite hivi hivi bila kuzingatia maoni ya wengi. Wakajiunga Ukawa washinikize "maridhiano" eti CCM wakubali "muafaka" ili Muungano uvunjike, CCM wakakataa. Zikapigwa kura, CCM wakashinda Ukawa wakatoka nje.

Tusitegemee CCM kutengeneza Katiba mezani iwasaidie CUF waliowashinda vitani, au CDM waliowashinda uchaguzi. Dunia ndivyo ilivyo, na CUF wakipata hawatoachia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…