Wapewe 'Second Chance'

Mwana

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
5,439
1,962
Kwanza nianze kwa kutoa pongezi nyingi kwa Serekali awamu ya tano kwa ufanyakazi wake wa uweledi chini ya Rais Mh. Dk. John Pombe Joseph Magufuli.

Lakini ningependa kutoa mapendkezo kuhusu hawa wanaovunjiwa nyunmba kwa kujenga mabondeni/ sehemu zisizoruhusiwa. Labda ningependa Waziri mwenye dhamana ya Ardhi kuna mambo ya kujiuliza kabla ya kuwavunjia nyumba hao waliovunjiwa. Kwanza sisupport kabisa kujenga sehemu zisizoruhusiwa lakini je Wizara ya Ardhi imepima viwanja vingapi? Je urasimu wa kuweza kupata viwanja vilivyopimwa umekwishatathminiwa????

Ninaamini kuwa wengi waliojenga maeneo yasiyoruhusiwa hutokana na kutokuwepo kwa hivyo viwanja vilivyopimwa. Aidha kuna taarifa nyingine kuwa hao watu walikwishapewa viwanja Mwabepande lakini wengi wao wamekataa. Sasa sio wakati wa kusema endapo wanadanganya au la kwa sababu kwa hivi sasa wako kwenye majanga huenda hata bei waliyouzia ni kwa ajili ya kujikimu tu kwa mwezi mmoja.

Nashauri Mh. Waziri sitisha zoezi kwa wiki 2. Wakati huo tafuta wataalamu wakusaidie kwanza kutathmini , halafu orodhesha wale woote wanaotakiwa kuvunjiwa, hakikisha wanapatiwa viwanja na hata ikiwezekana kwa kushirikiana na NHC wajengewe Nyumba za bei nafuu kwa mkopo wa miaka say 5( Chumba chumba Sebule ) wanaweza wakashirikiana na ile Taasisi ya Mama Siwale amabayo nasikia ilikuwa inauza nyumba za bei nafuu kwa wahitaji.

Kwa kifupi athari ya kuvunjwa nyumba inaenda mpaka kwa watoto ambao wengi wao wanafikiria hatma yao ya masomo. Najaribu kufikiria kama sio Programme ya Mkurabita watu ambao wangekuwa wanavunjiwa nyumba sijui wangekuwa wangapi, Programme hiyo imewezesha watu kumiliki nyumba kwa utaratibu maalumu pamoja na kuwa initially walijenga kwenye maeneo ya ‘squater’ Pamoja na kufuata sheria, athari za kuvunja nyumba hizo ziangaliwe upya na mpango wa kuhakikisha unapunguza madhara hayo uandaliwe na kutekelezwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…