Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,650
- 13,915
Uungwaji mkono wa Palestina umezidi kupaa kote duniani.
Huko Afrika kusini jioni ya jana Jumapili kikundi cha wanaounga mkono Israel kilikuwa kimeandaa ibada ya kuiombea Israel katika vita vyake dhidi ya Hamas na kuwaombea mateka wanaoshikiliwa huko Gaza.Shughuli hiyo ilikuwa ikiendelea kwenye eneo moja mashuhuri kwa mapumziko huko jijini Cape town.
Ghafla kundi kubwa la wapenzi wa Palestina wakabomoa geti na kuvamia eneo hilo,Wakavunja vunja mabango yaliyokuwepo eneo hilo, habari hiyo ikawavuta mamia kadhaa ya wapenzi wa Palestina na waungaji mkono Hamas kwenye mitaa.
Wakiwa wamevaa kofia za Hamas na kupunga bendera za Palestina wafuasi hao wakazidi kuwafurusha waungaji mkono wa Israel ambao walikimbia.
Baada ya hapo polisi ikabidi kuingilia kati kuzuia madhara zaidi yasitokee.