Doyi
JF-Expert Member
- Dec 4, 2011
- 1,574
- 1,882
habari wana jamvi?
Marehemu hasemwi vibaya wala mauti yakija hayana taarifa na siku yako ikifika bas hakuna wa kuzuia nafkiri hiz kauli tuishi nazo tu katika kujipa moyo chanzo chochote cha janga la kupelekea kifo kinapobainika.
ipo hivi wadau
kumetokea msiba ambapo mama mmoja ni jiran na maeneo nayoishi alikanyagwa na gari akapondeka kichwa na ubongo kutoka nje na akafariki hapo hapo.Ni mitaa ya bugosi wilaya ya tarime mjini mkoa wa mara ambapo mwanamama huyo ni shabiki kindakindaki wa CCM alishindwa kujizuia kushangilia ushindi wa uchaguz serikali za mtaa uliofanyika wiki iliyopita ambapo shamrashamra za vibe la kushangilia zilianza usiku.
Ila inadaiwa mumewe alimzuia asiende nje kushangilia kwa kuwa ilishakuwa usiku sana hivyo akamuomba asubiri ifike asubuh ili aendelee na hizo shamrashamra ila mwanamama hakuskia sauti za kanisa wala sauti ya mnadi swala akatoka nje usiku kushangilia ushindi ila bahati mbaya sana kuna gari ilikuwa ikitokea kenya imeshusha mzigo na wakat inarejea ikakuta kundi la wanaccm wakiwa barabarani wanashagilia inadaiwa ilipiga sana honi kuomba watu wapishe njia ila vibe la furaha lilimfanya marehemu adharau au asisikie honi zile(hatujui) ila liliwapitia watu kadhaa ambapo baadhi wamejeruhiwa viungo ila huyo mwanamama yeye alifariki pale pale hakuomba hata mma.
Naomba nisitaje jina lake kulinda privacy ya marehemu na familia yake ila kwa kweli ni simanzi nzito sana,wakat wa msiba inadaiwa mume wa marehemu alitamka hivyo kuhusu kumkanya mkewe kutoenda nje usiku na marehemu kukaidi...anyway siku zilifika lakin what if angemtii mumewe na kutoenda nje ?? wanawake biblia imewaamrisha muwe watiifu kwa waume zenu jaman ...anyway ni siku ya pili kama syo ya tatu tumeshamzika marehemu huyo na furaha ya chama chake kushinda uchaguzi imepeleka majonzi kwa familia.
ni hayo tu wadau
NB:Huenda habar hii ilishaletwa humu ila nimeiweka kwa upande wa pili wa funzo la utiifu hasa kwa wanandoa wanawake kuwatii waume zao.. am out