Habari wapendwa......
Hakuna ubishi kuwa Dar es salaam ni chem chem ya wasichana wazuri na warembo wa kila idara....
Ukikatiza mitaa ya mliman city, maeneo ya quality centre bila kusahau maeneo ya posta...hata sisi watu wazima huwa tunavunjika shingo kwa mshangao wa urembo wa hao mabinti.....unaweza ukajihisi ulifanya makosa makubwa sana kumuoa my wife wako na kumuweka ndani....maana unaweza ukahisi anakunyima uhuru wa kujivinjari na wasichana warembo....
Lakini bila ya kusahau kuwa hao mabinti tunaowaona kuwa ni warembo na wanavutia huko maeneo mbali mbali hawajashushwa mbinguni bali tunaishi nao huku mitaani......lakini kitu gani kinawafanya waonekane warembo wawapo posta mpya au maeneo mengine ya mijini kuliko wakiwa mitaani...??
Nimewahi kukutana na wadada kadhaa ninaofahamiana nao mitaani na wengine tukiwa tunaishi nyumba....lakini wote hao ilikuwa ni ngumu kuwatambua kutokana jinsi walivyobadirika....nyuso zina waka waka kama vile majini....hapo ndipo nilipogundua kuwa wanawake wengi wa jiji hili ni fake...kwa maana wana sura mbili mbili....
Unakuta mwanamke anaanzia nywele bandia ,kucha bandia, nyusi bandia ,kope bandia mpaka rangi ya mwili ni bandia...yaani kwa kifupi anapoteza kabisa uhalisia wake...sasa huyo ukiwa nae falagha unaweza ukamkimbia baada ya kuondoa hayo mataka taka yote....
NB; wadada wa jiji mbadilike hata kama ni kujiremba sio kwa kiwango cha mpaka unakuwa kama kinyago.....paka tu vikorombwezo vyako vya wastani tu....sio mpaka vinakubadilisha sura na kuwa mtu mwingine....