Wanawake tujirekebishe kweli wanaume wanavumilia mengi

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
26,574
48,723
Jumapili nilikuwa bored sana nyumbani nikatamani kutoka out nikamtafuta shosti wangu hivi kwa vile ni mnywaji nikamuambia twende nikakununulie kinywaji kimoja tupunge na upepo huko nje akasema poa akaniambia wewe tangulia mimi nitakuja basi nikaondoka na dogo mmoja wa jirani tukakaa mahali ila saa kumi na mbili nikamuambia dogo arudi nyumbani nikamuambia shosti vipi njoo akadai hana nauli eti atakuja na bodaboda anyway nikamwambia poa.

Akaja na bodaboda nikalipa tukaendelea kula bata kulikuwa na live band pale, akatoa order ya mzinga mkubwa na fanta mimi nikaaagiza tu maji yangu na kuchezacheza pale akamaliza akagiza tena mzinga mwingine na fanta na kuku choma mzima na chips eti anadai hajala toka asubuhi wakati alikuwa nyumbani mimi kanifata tu saa moja nikamwambia shosti nina elf 30 tu hapa nikamkabidhi kabisa nikaenda zangu kucheza, nimerudi kwenye meza nikakuta kamleta jamaa pale na mizinga imeongezwa miwili na chips kuku zishaletwa.

Huyo akaweka kwenye pochi akaniambia twende home mimi nikamuambia mbona time bado bahati mbaya alikuwa keshaanza kulewa kwahiyo ikabidi tu nikubali yaani kusema kweli nimeshindwa kuelewa ni ulafi au ni uswahili au ni nini mtu huwezi kutoka out ukanywa kitu chako kwa staha? Unatoa order kama unakomoa?

Nimekoma mwenzenu bora nijifungie ndani nichat tu JF kama kaka yangu RRONDO ila nashukuru Mungu nilipata mitongozo ya kutosha ikanipa matumaini kwamba sijazeeka sana mi mwenyewe tu sijiamini.
 
Pole sana miss natafuta na huu usawa ulivyo mgumu mhhhh sipati picha, mie hayo mambo ndio sitaki nashukuru Mungu kanipa marafiki tunaofanana akili, tukitoka out bili tunagawana sawa kwa sawa na hakuna chain na ukiita mtu wako bili yake juu yako uliyemuita, hatutakagi ujinga kabisa. Na kila mtu anajua rules and procedures zetu.
 
nilipopenda ni hapo tu uliposema hujazeeka sana haya mamii endelea kula bata kwani uzee haupigi hodi ujue.
 
FALA SANA KAPOTEZA BAHATI ANGEBEHAVE ANGENIFAIDI SANA
achana nae huyo hana maana ukitaka kampani niambie nije kula samaki au kitimoto ya kuchoma na nikitolewa out naongea mimi mpaka utafurahi sema story nyingi za uongo na nyingine za jf najipa uhusika mimi basi full burudani... sema wine lazima na usishike shike simu yako basi tutaenda sawa
 
SIO RAFIKI YANGU KIIVO HATA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…