Mimi binafsi nikiri kuwa na mpenzi na shabiki mkubwa wa mpira wa miguu na michezo ya mieleka, kwa wale wanaofatilia mpira wa ulaya kuna mechi za katikati ya wiki huwa zinachezwa usiku sana mara nyingi huanza kama si saa nne na dk 45 basi saa tano kamili usiku.
Nilikuwa lazima niende kwenye mabanda ya video au bar kuangalia kitu ambacho nilijua na kushuhudia kikimkera sana mpenzi wangu japo alikuwa ananiruhusu niende nilikuwa namwona hana furaha nikajionja nikasema huu mpira utakuja kuvunja ndoa yangu.
Nikajichanga changa nikaamua niende kununya DSTV ili niwe naangalia nyumbani mpenz wangu alifurahi mno siku naenda kununua nikakuta kaenda kununu kuku wa kienyeji akasema leo mme wangu ninafuraha sana akatengeneza juice ya embe nikamwona mda wote anafuraha na kukaa karibu yangu.
Nikamwambia kulipia kifurushi kikubwa hicho unaangalia mechi zote ni 184000/= akaniambia we unashilingi ngapi nikamwambia nimebaki na 100000 tu Akaingia ndani akanipa 100000 akaniambia keep change, mke wangu namjua bahili sana siyo kutoa laki haraka haraka ndipo nilipojua nilikuwa namwumiza sana.
Sasa napenda nisaidiwe wanawake mnaumia kwa kiwango gani tunapotoka kwenda kuangalia mpira usiku? Huku mkijua waume zenu ni wanazi wa kutupwa wa mpira.