Hahahaaa...
Hatukatai kuolewa ni haki yako, lakini jiangalie hata staha yako, wewe utakua ni mke gani ndani ya ndoa jamani, toka uzaliwe hukumbuki kanga wala sketi ulivaa lini na kama ulivaa kanga basi ni style ya kanga moja.
Duh! Mtoto wa kike unaishi kama msela we na viduku kutwa kucha alafu eti una ndoto za kuwa mama wa familia, kwa malezi yapi? Tahadhari dada zangu sharobaro haoi kazi yake ni kugusa tu.
Hebu jiweke kama binti mwenye malezi ya pande mbili uone kama hutapendwa, usipokua makini utaishia kuhudhuria send off na harusi za wale unaowaona wanaishi kishamba kila siku.
Ukinuna imekugusa, naomba kutoa hoja