Alex Tanzania
JF-Expert Member
- Jul 8, 2016
- 782
- 646
rubi.Mh umenikumbusha mbali wewe ndugu, Kuna mioyo inamiliki siri kubwa sana kwenye jamii zetu....hata hivyo malipo ni duniani akhera hesabu tu
Tusamehane tu...unaweza ukaa kaa na mtu na ukamchoka.....wengine wanaogopa kusema.....basi wanayaacha tu mwisho uwe vyovyote vile.......Ninamfahamu dada mmoja aliishi na jamaa tena walifanikiwa kupata mtoto, kila wakikaa jamaa anasema hayuko tayari kuoa, ohh kwanza nikasome Masters , mradi mwenye lake hakosi neno. Yule dada mwisho aliona kabisa namba haisomeki. Aliondoka lakini uzuri alikua na elimu yake. Alitua kwa mama kwanza, akajipanga vizuri, kabla hata hajakaa sawa, anasikia harusi jamaa anaoa. Inawezekena kabisa jamaa alipata mchumba wakati bidada yuko ndani bado. Yakitokea ni kumshukuru Mungu kwani kisicho rizki hakiliki.
Na kama umemuoa kisheria utafanya nini ukimchoka?Tusamehane tu...unaweza ukaa kaa na mtu na ukamchoka.....wengine wanaogopa kusema.....basi wanayaacha tu mwisho uwe vyovyote vile.......
ukimchoka si unamwambia kuliko kutoa visingizio.........na kumpa fake promise etc.Tusamehane tu...unaweza ukaa kaa na mtu na ukamchoka.....wengine wanaogopa kusema.....basi wanayaacha tu mwisho uwe vyovyote vile.......
ataendelea na vituko mpaka mweyewe uchoke uondoke........Na kama umemuoa kisheria utafanya nini ukimchoka?
Pole sana ''rubii'' wangu, ndo maisha yalivyo. Samehe 7 mara 70, na Mungu atakulipa.Mh umenikumbusha mbali wewe ndugu, Kuna mioyo inamiliki siri kubwa sana kwenye jamii zetu....hata hivyo malipo ni duniani akhera hesabu tu
Pole sana ''rubii'' wangu, ndo maisha yalivyo. Samehe 7 mara 70, na Mungu atakulipa.
Nimekuelewa......lakini iliyopo hiyo ni kwamba bado ni wachumba....Ila kama mtu ulioa kabisa legally hafu unazingua hiyo ni mada nyingine aiseeeee.......Na kama umemuoa kisheria utafanya nini ukimchoka?
talaka si ipo.......huna hisia nae wa nini sasa...!!Na kama umemuoa kisheria utafanya nini ukimchoka?
mkuu naona umewapendelea sana wadada, inshort hata wao wana makosa makubwa sana. men cheat women cheat tooHabari wana JF,
Naomba niwashirikishe hili kwa uchache.Itasaidia kiasi fulani.
Yawezekana nimepost hili kutokana na woga wangu lakini nimeshuduhudia visa vitatu vinavyofanana katika mahali ninapotoka (mkoa) ingawa vilitokea katika maeneo tofauti (wilaya).
Ni hivi, kuna hii tabia ya wanaume kuwa na uchumba (kwa maana ya kwamba mpaka wazazi wa pande mbili wanakuwa wanafahamu) na mtu fulani then baadaye kumuacha mwenzako bila sababu ambazo hukumwambia (yawezekana zikawa zina mantiki au zikawa ni povu tu).
Sasa kwa hivi visa nilivyoshuhudia (kwa maneno ya watu/tetesi kutoka kwa watu wa karibu) matokeo yake ilikuwa ni vifo kwa wanaume waliofanya hivyo (vifo hivyo vilitokea ghafla na katika mazingira yenye maswali mengi) na kuonekana kwamba waliofanya hivyo ni upande wa mwanamke (huku mhusika akihusika kabisa au mhusika asijue kabisa ila wazazi wake wakashiriki).
Sasa nichouma zaidi ni kwamba unaachwa huambiwi sababu halafu baada ya muda mfupi unasikia kuwa mwanaume uliyekuwa nae anaoa mtu mwingine (ambaye sio wewe), ukizingatia mlishapanga mambo mengi ya baadaye katika maisha yenu ya baadaye (though uchumba sio lazima mfike katika ndoa, kinacholalamikiwa hapa ni taarifa).
Sasa hii ni visa viwili kati ya hivyo vitatu. Cha tatu ni kwamba jamaa alicheza na hisia za mdada wa watu alimtumia/walitumiana walivyotaka then jamaa baadaye akamuacha kwa dharau bila kutoa sababu, mwezi mmoja baadaye jamaa alipata ajali katika usafiri wa jamii na alipoteza peke yake.
Hitimisho ni kwamba wote hawa walikufa katika mazingira ya kishirikina (taarifa kutoka mtaa kwa watu wa karibu). Pia kwa vijana wenzangu taarifa ni muhimu unapotaka kuachana na mwenzako (tengeneza tu mazingira au mtafutie sababu kidogo anaweza akaachika ila sio kumkomoa kwa kutoka na wengine (ingawa najua hili halizuiliki though wadada huwa hawajui/hawaamini-lakini sio sifa). Pia kwa wadada mliokutana na haya nawapa pole.
Amani kwenu.
Nawasilisha.