figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,620
- 55,261
Hivi karibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa Mkoani Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya TAMISEMI, alisema jumla ya watanzania 31,282,331 wamejiandikisha kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024, ambao ni sawa na asilimia 94.83 ya lengo la kuandikisha wapiga kura 32,987,579.
Aliongeza kwamba Watanzania wanaume waliojiandikisha ni 15,236,772 sawa na asilimia 48.71 na wanawake ni 16,045,559 sawa na asilimia 51.29 ambao kwa mujibu wa kanuni na sharia ndio watashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu,” Mhe. Mchengerwa ameanisha.
Shime Wanawake wa Tanzania, huu ndo wakati sahihi wa sauti zenu kusikika kwa kushiriki katika ngazi za Maamuzi kuanzia Serikali za Mitaa kwani Uchaguzi huu unaonesha Uchaguzi Mkuu wa 2025 Utakavyokuwa.
Hivyo ni jukumu la Kila Mwanamke kuhahihisha anagombea na kupiga kura.
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019, wanawake waliogombea walikuwa asilimia 33 ya wagombea wote. Hivyo Mwaka huu inatakiwa hii idadi iongezeke
Dhana ya 50 kwa 50 wanayoitaka kwenye jamii hawezi kufikiwa kama Wanawake wasipojitokeza kugombea. Hivyo ni wajibu wa kila mwanamke kuchukua fomu na kuingia kwenye ushindani kwani Mwanaume na Mwanamke akili wote wana akili na wote wanaweza kufanya maamuzi sawa, hivyo hii ni fursa kwao