Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 3,017
- 5,508
Moja kwa moja kwenye mada taja hapo juu, kumekuwepo na malalamiko kadhaa katika baadhi ya ndoa ama mahusiano. Malalamiko hayo ni baadhi ya wanaume kupewa watoto wasio wao, inatokea mwanaume anahudumia mimba ya mke wake ama mpenzi wake mpaka kujifungua mwisho wa siku inagundulika mtoto sio wake. Ama mwanaume kulea mtoto/watoto akiamini ni wake kumbe amepigwa na kiti kizito.
Leo nimekuja na mbinu mbadala kuepusha janga hili ambalo linaumiza na kutatisha tamaa. Mwanaume ukiwa tayari kwa kupata mtoto na mpenzi wako itakubidi utumie mbinu hii ili kuepuka kupigwa na kitu kizito. Endapo uko tayari kwa mtoto kwa mwaka husika andaa miezi yako miwili kisha nenda ata ushagoo(kijijini) kwa mapumnziko na mpenzi wako. Sio lazima kijijini popote pale utako ona ni sahihi kwako.
Kabla ya kwenda hakikisha kuwa ile siku mnaanza safari yenu kuelekea huko mtakako amua wenyewe, mpime mpenzi wako kipimo cha ujauzito na uhakikishe kipimo kinasomo hana ujauzito wowote ule. Pia unapaswa uujue mzunguko wa hedhi wa mpenzi wako kwa ufasaha zaidi. Kisha baada ya hapo fanya maandalizi ya safari, hakikisha katika mizigo yako unachukua vipimo vya kupima mimba vya kutosha.
Mkifika huko mliko amua kuweka kambi ya miezi miwili hakikisha huko mpenzi wako na wewe hamtoki kwenda sehemu yoyote yaani mshindi pamoja kila wakati na kila mahala. Kumbuka hapo mpo kwa ajili ya kutafuta mtoto wako wa halali sio wa kubambikiwa. Furahini penzi lenu huku mkipiga shoo za maana, kumbuka kufanya vipimo cha ujauzito kwa mpenzi wako mara kwa mara. Ndani ya miezi miwili kama hamna shida yoyote ile ya kiafya mimba itakuwa imetungwa panapo majaliwa.
Baada ya mimba kutungwa sasa mnaweza rudi mliko toka kuendelea na pilika nyingine. Hapa mwanaume utarudi ukiwa na uhakika mkubwa kuwa kile kitakacho zaliwa ni kiumbe chako halisi bila kupepesa macho.
Kila la kheri kwenu nyote.