Ukisha kuwa na negative attitude juu ya mume wako, hakika utampoteza, mwisho wa siku unakuwa wewe ndio uliyemtoa kwa wenzako huko. Unachotakiwa kufanya ni wewe kutimiza wajibu wako, I am sure mume atakuwa mwaminifu almost 100% kwako na familimia yake.
Ila ukianza kusema ahaa wanaume sio waaminifu, mwisho wa siku hutotimiza wajibu wako kwake na familia, lawama nk, mwisho wa siku kidogo kidogo unamuweka mbali na wewe na akiwa huko nje akiona mke mwingine mzuri machoni pake anashindwa kukumbuka kuwa kuna kifaa kingine adhimu amekiacha nyumbani, taratibu uaminifu unazidi kupungua hadi unampoteza mtu wako wa thamani, lakini chanzo ni wewe mwenyewe pasipo kujua hilo.