Wanaume na wanawake mnaotaka kuoa au kuolewa, pitieni haya mamabo 5 ili mjiandae kisaikolojia

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,551
22,097
Habari enyi wapendwa!

Karibuni katika tafakari ya changamoto ndogo ambapo mtu huweza kukutana nazo punde tu aingiapo kwenye ndoa ama aishipo kama mme na mke; Katika mahusiano ya uchumba/ girl na boy friend mapenzi huwa matamu sana, mapenzi haya hukua na kukua hadi kufikia hatua ya kuamua kuoana kabisa ili muanze maisha ya ndoa. Lakini Kabla hujaingia kwenye ndoa hiyo naomba ujiandae kisaikolojia kukabiliana na mambo kadhaa wa kadhaa ambayo hutokea na mara nyingi huanza kuyumbisha familia taratibu taratibu hadi kuvunjika;

1. Kuna hili jinamizi la kuporomoka kiuchumi kwa wanandoa- waliochunguza watakubaliana na mimi kwamba wana familia wengi punde tu wanapoingia kwenye tasnia hii hukumbwa na dhoruba Fulani la kuyumba kiuchumi, yaani utashangaa mtu anakosa kabisa pesa ya kujikimu kiasi kwamba hadi watu ndoa huziona ni chungu kipindi hiki, yamkini waweza kuwa chanzo ni biashara zako kuyumba, kufukuzwa kazi n.k- hali hii huwa inakuja kwa mda wa miezi kadhaa ambapo isipotaftiwa ufumbuzi huvunja kabisa ndoa.

2. Changamoto ya pili ni pale ambapo mkeo hupata ujauzito wakati wewe huenda upo katika hali mbaya sana kiuchumi, yaani zile OUTING za kipindi cha uchumba kwa mkeo hazipo, kipindi hiki mwanamke huhitaji uangalizi wa hali ya juu na pengine mke hutamani vitu kadha wa kadhaa ambapo kwa wakati huo wewe huna kabisa uwezo, yawezekana hata ile milo mitatu inakushinda kumhudumia kutokana na kuyumba kwako kiuchumi. Wakati huwa mgumu zaidi pale mkeo ataanza kukulaumu kwa kila kitu unachokifanya kwamba haoni faida yake. Jambo hili huwafanya wanaume akili iruke kabisa kwa kuwaza wafanye nini, wengine hutoweka nyumbani na kwenda mbali ili wakwepe hilo GUBU la kusemwa ama kuombwa hela ya kula nyumbani angali hawana kitu.

3. Changamoto ya tatu, ni pale mkeo anapojifungua, yamkini ukawa mvumilivu sana katika ndoa yako, lakini katika kipindi hiki mkeo anapojifungua hiki ndiyo kipimo sahihi cha kujuwa uvumilivu wako, Achilia mbali zile siku arobaini za mama anazotumia kupona Bali kuna changamoto ya ladha Fulani hupungua sana, kwanza mkeo huwa katika hali Fulani tofauti na alivyokuwa katika usichana wake, maziwa hutepeta, tumbo hutepeta na kunako K-papuuch nako huwa kama kunapwaya, kiasi kwamba kama ulizoea kupiga bao 3, basi lazima utaishia kupiga kamoja tu tena kwa mbinde; Note; wakati huo mwanamke huwa hayupo kwenye hamu kabisa ya tendo hilo na wengine hujiona inferior na kujiona kama thamani ya uzuri wao hupungua n.k KIPINDI HIKI NDIPO MWANAUME HUANZA KUCHEPUKA ASIPOKUWA MVUMILIVU

4. Changamoto ya nne; ni hiki kipindi cha malezi ya mtoto yaani miezi 1 hadi 5, kipindi hiki mtoto husumbuliwa na magonjwa kadhaa ya watoto- wakati huo huo mara nyingi hawa watoto hulia sana hasa mida ya usiku hamlali, yaani hapo huwa ni mwendo kubadilisha nepi na kubembeleza mtoto asilie usiku kucha(kipindi hiki wengine hufikia hadi kupewa notisi na wenye nyumba maana huwa hapalaliki) na endapo ni kipindi cha mvua kumbuka kwamba matambala ya nepi kwa mtoto hayakauki, pia pambasi yamkini pesa huna hapo huwa ni shida kabisa. IKUMBUKWE pia wakati huu mara nyingi huwa ni marufuku kuwasha AC/FENI ndani kwa ajili ya mtoto asipatwe na Pneumonia, kwa maana hiyo hata unajitambi kubwa kiasi gani inabidi uvumilie JOTO…KIPINDI HIKI NDIO WANAUME WENGI HUWAPELEKA WAKE ZAO MAKWAO KWA VIZINGIZIO KADHAA KAMA KUJISIKILIZIA, KUPUMZIKA n.k, YOTE HAYO NI KUKWEPA MAJUKUMU HAYO.

5. Changamoto ya tano; KUBEMENDA MTOTO, hii kitu kisayansi madaktali ni kama hawaitambui, lakini hii kitu ni hatari sana; Hapo mama akimwagiwa shahawa ndani mara nyingi huleta madhara kwa watoto wanaponyonyweshwa, na baba unapochepuka halafu uje ulale na mkeo yaweza ikawa chanzo pia cha kumbemenda mtoto, (mtoto hatembei) na mara nyingi aibu hii humpata mama wa mtoto kusemwa na wanawake wenzake; mtoto vi-miguu huwa vidogo sana hadi anatia huruma ambapo tiba yake watu wazima wanaijua.

Hizo ni baadhi tu ya changamoto ambazo wewe unayejiandaa kuoa/kuolewa Tegemea siku utakutana nazo na anza kujiandaa KISAIKOLOJIA ili isiwe chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yako; NOTE; Endapo Mukifanikiwa kuvumilia hiyo mitihani yooote,Basi ndoa baadaye huja kuwa taamu sana maana hutokea neema ya ajabu sana ambapo kazi utapata tena nzuri, Biashara nazo huanza kuleta mafanikio makubwa, mtoto hukuwa na kuwa burudani ndani ya nyumba!
Updates;
Kwakweli pia zipo changamoto zingine nyingi mbali na hizo kama mimba kuharibika,vilema na magonjwa Kwa wanandoa, kuzaa njiti au kuzaa watoto mapooza au wafu n.k Hayo yote yanahitaji uvumilivu sana katika ndoa na hatimaye familia bora.
Mwisho
(Natanguliza shukrani sana kwa baadhi ya wanawake wanaotelekezwa na waume zao na kuachwa na watoto wao bila msaada na wanalea hadi mtoto anakuwa...na cha ajabu WANAUME WENGI HURUDISHA MAPENZI YAO HASA HASA WANAPOONA MTOTO KAFIKISHA 2YRS +)..Karibuni sana.
****Madhara ya kuchepuka huleta watoto wa nje ya ndoa na magonjwa*****
 
good observation ila zipo sabab nyingine ndogo ndogo ambazo pia ni hatari...
 
Points zako zote umeenda vizuri na ninakupongeza kwa hilo.

Tatizo lipo kwenye point namba 5 inayohusu kubemenda.

Kama ulivyokili,kwamba madaktari na sayansi hawatambui kitu inaitwa kubemenda na ukweli ndiyo huo kwamba kubemenda ni jambo la kiimani tu na halipo kisayansi.
 
Zipi hizo ziweke hapa
Gugu,uchoyo,dharau,kiburi,ulevi,kutoheshmiana,tamaa nk hizi ni sababu ambazo mara nyingi hazionekani kwa haraka kutokana na udogo wake but zikikomaa ni bonge la kansa kwenye ndoa.mara nyingi wakati wa uchumba huwezi kuziona hizi kitu coz kila mtu anajitahidi kizificha.but si unajua tabia hauwezi kuificha milele? ukisha ingia kwenye ndoa sasa ndo zinaanza kujichomoza taratibu usipokua mjanja mzee utaumia.
 
Sasa kinachotokea Kwa mtoto huwa ni nini? Waweza kutusaidia somo hilo?
 
mtoa mada uko vizuri. sio lazima watu wote wapitie haya au kila mtu apitie haya yote unawezankukumbana na baadhi yake kati ya haya.
 
Umeshawahi ona tatizo la mtoto kuwa na vimiguu vifupi (mtoto alie bemendwa) kwenye familia zenye uwezo kiuchumi/tajiri?
 
Umeshawahi ona tatizo la mtoto kuwa na vimiguu vifupi (mtoto alie bemendwa) kwenye familia zenye uwezo kiuchumi/tajiri?
Familia nyingi zilizoendelea ni chache sana halafu watu wake wameelimika mkuu.
 
mtoa mada uko vizuri. sio lazima watu wote wapitie haya au kila mtu apitie haya yote unawezankukumbana na baadhi yake kati ya haya.
Umeona eeh; yapo mengi sana siyo lazima yawe hayo....kuna changamoto ya Mimba kuharibika nalo huwa ni balaa sana hilo .
 
Wewe unafikiri wameelimika katika lip? Sorry but!!!
Ngoja nikupe ufafanuzi kidogo; katika Jamii ya kawaida kubemenda hakutokei Kwa kila mtu,huwa ni nadra nadra sana, yamkini kwakuwa hupeana elimu; na hii Jamii ni kubwa kuliko Kwa matajili. Sasa kama matajili ni wachace basi hata matukio kama hayo naimani ni machache sana kiasi kwamba ni ngumu kuyaona hats hivyo wengi wao wanaelimu ya uzazi na afya ya mtoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…