Mshangazi dot com
JF-Expert Member
- Nov 19, 2011
- 783
- 1,878
Jamii zetu za kiafrika zimeweka mzigo mkubwa sana kwa mwanaume.
Naomba kutambua mchango wenu na kuwapa maua yenu kama ishara ya shukrani.
Shukrani za dhati ziwaendee;
🌹 Wanaume wanaoweka juhudi katika kazi zao halali, wakifanya kwa uaminifu na kujituma ili kujenga maisha bora kwao na familia zao – pokeeni maua yenu.
🌹 Wanaume wanaopambana kuhudumia familia zao bila kuchoka na kulea watoto wao kwa mapenzi na maadili mema – pokeeni maua yenu, tunawashukuru.
🌹 Wanaume wanaoshikamana na marafiki zao kwa uaminifu, kusaidiana katika shida na raha, na kuwa nguzo ya kweli kwa wenzao – pokeeni maua yenu.
🌹 Wanaume waliotoka kwenye maisha magumu na wanapambana kila siku kuhakikisha vizazi vyao vinaishi maisha bora kuliko wao – pokeeni maua yenu, tunawashukuru sana.
🌹 Wanaume wanaopambana na changamoto za afya ya akili kimya kimya, wakitafuta suluhisho bila kukata tamaa – pokeeni maua yenu, tunawatambua na kuwathamini.
🌹 Wanaume waliowahi kupitia maumivu makali (kuachwa, kupoteza wapendwa, kufeli, kuumizwa) lakini bado walisimama tena na kusonga mbele – pokeeni maua yenu!
🌹 Wanaume wanaopambana na hali ngumu za maisha bila kulalamika na bado wanajitahidi kutokata tamaa na kutia wengine moyo – tunawashukuru, pokeeni maua yenu.
🌹 Wanaume wanaosimamia shughuli za kijamii; likitokea tatizo wao ndiyo mstari wa mbele kupambana (mwizi mtaani wamo, misiba, sherehe, n.k.) – pokeeni maua yenu na asanteni sana.
🌹 Wanaume wanaolea watoto wa wenza wao bila kuwabagua na kuhakikisha wanasimamia nafasi zao kama wazazi wenza – pokeeni maua yenu.
🌹 Wanaume wanaohakikisha wazazi wao na wale wa wenza wao wanatunzwa na kuheshimiwa – tunawashukuru, pokeeni maua yenu.
🌹 Wanaume wanaowapenda, kuwaheshimu, kuwalinda na kuwasaidia wenza wao – pokeeni maua yenu na asanteni sana.
🌹 Wanaume wanaopigania maslahi ya wananchi na wanajamii wenzao, kuhakikisha usawa na haki zinazingatiwa kwa kila mmoja – tunawashukuru sana, pokeeni maua yenu.
Leo ni siku yenu, hasa wale wanaume wanaojituma na hawapati "ASANTE" wanazostahili. Shukrani kwa yote mnayofanya na kutufanyia 💐✨.
Ongeza na wewe sababu za ziada za kuwapa maua yao wanaume wa shoka kwenye jamii na maisha yetu.
PS:
Wale mnaopwaya pwaya hii nyuzi haiwahusu, ila mnaweza kujifunza kutoka kwa wenzenu.