Mwanaume anaweza kuwa mcheshi na mwenye kuvutia pele ambapo anataka kukusogeza uingie kwenye mtego wake kwa miguu yote miwili.
Kwa harakaharaka anaweza kuonekana mkamilifu kumbe ana taswira tofauti inayokinzana na uhalisia wake, mwanaume anaeonekana mkamilifu mwanzoni kabisa kwenye mahusiano anaweza kuwa miongoni mwa wanaume hatari kuwa nao.
Leo nakuletea aina ya wanaume ambao kamwe hutakiwi kuvitiwa kuingia nao kwenye uhusiano.
Mwanaume anaeonekana mkamilifu anayeishi peke yake bila mchumba wale mke. Unashangaa kwanini mwanaume mkamilifu kama huyu mpaka leo hajampata mwanamke wa kuishi nae? unafurahi kupata nafasi ya kuwa nae. Mwanaume wa hivi atakufanyia mambo mengi mazuri atakupa hela, atakununulia vitu pengine hata kukutafutia kazi lakini Kuna siku mambo yatabadilika kidogo tu atakukimbia utabaki unajiuliza kumbe ndio maana nilimkuta yupo mwenyewe.
Mwanaume aliye tayari kukuoa kwa kushitukiza ni miongoni mwa wanaume hatari kuwa nao. mwanaume wa namna hii anakuwa tayari kukuoa tu kwa mara ya kwanza mnapokutana. yeye hufikiri kuwa ndoa ni hatua rahisi ambayo inaweza kutokea wakati wowote na popote lakini atakapokuoa tu mapenzi yataisha kwa muda mfupi ataanza biashara na mtu mwingine mgeni kwenye macho yake.
Aina nyingine ya wanaume unaopaswa kuwaogopa ni wanaume wenye kupenda maonyesho ya ufahari na pesa. Wanaume wa aina hii hupenda kuongelea maisha mazuri, nguo nzuri, simu na sherehe za gharama kubwa lakini kiuhalisia hawana pesa wanajaribu tu kukuteka ikiwezekana watumie pesa zako.
Watoto wa mama. Hii ni aina ya wanaume ambao hawamsikilizi mtu yeyote isipokuwa mama yao. Wana mihemko sana ya kutegemea mama zao na kama ikitokea mwanamke akaingia kwenye uhusiano na mwanaume wa hivi basi atakosa nafasi kwa sababu tayari kuna watu wawili na yeye atakuwa mtu wa tatu lakini hawezi kufurahia maisha ya mwanaume wake.
Mwanaume asiyeweza kuwa siriasi. Mwanaume wa aina hii hawezi kuwa siriasi kwenye hali ambayo unahitaji msaada wake na muda, yeye atakuwa bize kwenye matukio kama sherehe au kwenda klabu, atakuzalisha watoto lakini atakosa muda wa kuwalea kama baba.
Β© Peter Mwaihola
View attachment 3217294wanume