Kiburi si uungwana
Member
- Sep 6, 2018
- 88
- 274
Kwa siku za karibuni kumekuwa na tabia kwa wanasiasa kuanza kuingilia uhuru na haki yetu ya kuchagua maisha ya kuishi na ambayo hayavunji sheria za taasisi yoyote.
Kutokana na matukio ya kimihemko ya baadhi ya vyama kutopata ushirikiano kwa raia ambao walidhani maisha yao yanaendeshwa na mihemko, baadhi ya wanasiasa wameanza kuingilia uhuru wa raia wa kuishi maisha yao.
Wameanza kuona chochote ambacho kinachukua nafasi kwenye akili za raia wa nchi hii kuwa ndio kinawanyima fursa kwenye kumfanya raia huyu awaze kile wanachojaribu kutaka afanye.
Imefikia hatua baadhi ya mambo kama michezo na burudani kuonekana ndio chanzo cha kufanya raia wajisahau na kutozingatia kuzungumzia mambo ya maendeleo ilhali wao kama wanasiasa ndio wana jukumu na uwanja wa kuonyesha kipi kifanyike na wapi kufanyike kwa mujibu wa utaratibu, badala ya kutimiza majukumu yao, wanasiasa wetu wamekuwa watu wa siasa za matukio badala ya maendeleo.
Naomba msitupangie maisha wanasiasa, kama mmeshindwa kuonyesha mwanga kwenye kupigania maendeleo yetu basi mtuache tuendelee kujifariji na haya mampira ya simba na Yanga na nyie endeleeni kupigania huruma zetu badala ya maendeleo alafu muone kama kuna mtu mwenye akili timamu atawaunga mkono, na mkajifunze umuhimu wa michezo na burudani kwa raia.
Tuna maisha magumu ni kweli ila mmeshindwa kazi, wanaokula waacheni wale, tukichoka tutafanya ya bangladeshi na srilanka, tutaenda wenyewe ikulu na wengine tutaenda bungeni kama wenetu wa kenya a.k.a Gen Z