Katika kampeni za mwaka huu kuna jambo ambalo wanasiasa wamekuwa wakiwahadaa watanzania na watu wamegeuzwa mashabiki bila wao kujua. Wamesikika watu wakisema kuwa Tanzania inahitaji elimu ya bure. Maneno kama haya ni sawa kuyatamka kisiasa lakin sio sawa kiuhalisia.
Changamoto yetu kama taifa ni elimu iliyo BORA ambayo mtu akimaliza shule ya kata ubora wake uwe sawa na mtu alietoka St Mary's Feza,Tusiime,St Mthew n.k . ifike wakati kuwa mtu kwenda shule binafsi kma nilizotaja hapo liwe ni suala EXTRA na STAREHE kama vile ilivyo kununua bia kwenye kibanda cha Mangi na kunywa na kuwa sawa na aloenda Serena kunywa bia maana zote ni bia na ukizinywa utalewa.
Ni utoto kusema mtu asomeshwe bure mpaka chuo kikuu huku kichwani akawa amekaririshwa mitihani na mchango wake kwa ukuaji kiuchumi ukawa zero. Elimu yetu imeporomoka kwa kasi sana kwa sababu wanasiasa wanamini kuwa kujenga shule nyingi za sekondari na vyuo vingi vya elimu ya juu ni kupandisha thamani elimu yetu kumbe wanaidumaza huku sisi tukigeuzwa kama chapatti na kushangilia mambo bila kuyatafakari. Lengo sio upatikanaji wa elimu kwa watu wengi; lengo kubwa sasa liwe ubora wa hiyo elimu wanayopewa hao wanaomaliza ili wakiingia kwenye soko la ajira wapambane kisawasawa na washindani wetu kitaaluma.
Ni aibu kwa taifa hili kusema kuwa tunahitaji elimu BURE ambayo haina ubora wowote kitaifa na kimataifa. Elimu ambayo mwajiriwa anapata kigugumizi kukuajiri ;elimu ambayo watu hawafundishwi practise ila wanafundishwa theory. Elimu sasa isiwe quantity kwamba kila mmoja akasome ila elimu sasa ibadilishwe kuwa quality. Ni afadhali elimu ikawa quailty and free kuiliko kuwa quantiy and free.
Wanavyuo vya elimu ya juu wapatiwe msaada na wawezeshwe kwagharama a ada na malazi na kila stahiki bila kucheleweshwa.Ila wanachokisoma kiwe bora katika soko la ajira.Elimu ibadilishwe na kuleta watengeneza ajira na suio watafuta ajira maana elimu ya bure bila pahala pa kumwajiri mhitimu ni sawa na kulima kwenye lami. Kwa sababu hawa waakuwa mizigo kwa serikali na waaendelea kusema serikali haijaufania kitu.
My take, tupime sera za wanasiasa hawa kwa uhalisia na sio kwa ushabiki na mahaba ambayo yatakuja kutupoteza kwa miaka kumi ijayo. Sidhani kama tunataka elimu BURE ambayo sio BORA.
PIGANIA ELIMU BORA MWAKA HUU