Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,072
- 4,508
Tumejifunza mengi kutoka kwenye munyukano wa kisheria uliotokea kwenye Mahakama Kuu ya Mbeya kuhusiana na mkataba kati ya DP World na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tulichoshuhudia ni tofauti kabisa na kile ambacho baadhi yetu walikuwa wametuaminisha kwamba wanasheria wetu ni vilaza watupu na ndiyo sababu ya kuwa na mikataba mibovu na kushindwa kesi za kimataifa huko ICSID na kwingineko.
Tumeshuhudia jinsi wanasheria mawakili wa pande zote mbili walivyo na weledi mkubwa wa ku convince na ku confuse in a professional manner katika kuchambua sheria. Tumejifunza kuwa Katiba yetu ya nchi imempa Rais sovereign (aka supreme) power ya kufanya chochote ikimpendeza. Sovereign powers hizo wananchi humkabidhi kwenye uchaguzi mkuu.
Tumejifunza kwamba hicho wanasiasa wanachokiita kuuzwa kwa bandari zetu si kuuzwa in the literal meaning bali ni kuwapa hawa DPW sovereign powers ya bandari zetu zote. Tumepoteza sovereign powers zetu kwenye bandari zote na special economic zones.
Tumejifunza kuwa wabunge ndiyo wawakilishi halali wa wananchi. Na bunge huendeshwa kwa kanuni iliyojiwekea. Hao wadau si wawakilishi rasmi wa wanainchi, kuhusishwa kwao ni kwa kanuni tu za bunge, idadi yao na muda wa notisi ni kwa mapenzi ya Spika.
Kila fani (profession) vilaza huwaga hawakosekani. Kuna madaktari vilaza, waalimu vilaza, wahandisi vilaza, wanahabari vilaza, wanasiasa vilaza na kadhalika. Wahenga walishasema kwamba kwenye kundi la mamba, kenge huwa hawakosekani.
Tatizo letu huwa tunatafuta wale wanasheria vilaza aka kenge kututengenezea mikataba yetu, hivyo kuwa na mikataba mingi mibovu inayotusababishia kushindwa kesi huko ICSID.
Tatizo letu huwa mara nyingi tunachagua wanasiasa vilaza kuwa wabunge wetu na hivyo kusababisha mikataba mibovu ilidhiwe faster faster na kadhalika. Ila ikumbukwe rushwa ina uwezo wa kumfanya mtu ye yote mwelevu akaonekana kilaza wa kutupa. Money is the source of all evils and not the devil!