Wanasheria naombeni msaada wenu

Amocnolo

Member
Oct 16, 2023
23
26
wanafamilia moja wamekuja kwangu wanataka wagawane mali walizochuma ndipo nikaomba kujua historian yao hadi kufikia hapo, ipo ivi.

Ilikuwa 2018 mahusiano yao yalianza na wakati huo mwanaume alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni moja aliajiriwa, ilipofika 2019 alifukuzwa kazi na kipindi chote icho walikuwa kwenye mahusiano na huyo binti alikuwa mjamzito na anaishi kwao, huyu mwanaume alikuwa na akiba kidogo bank akachukua hiyo hakiba yake akanunua pikipiki ili kuendesha maisha hadi yule mwanamke akajifungua wakati huo mwanaume bado anasubiri peza zake za ppf,

2020 yule binti akajifungua mtoto wa kiume, akaamua kumchukua na kuishi nae lakini hakumuoa wakawa wanaishi tu, pesa za ppf zilipotoka yule mwanaume akaamua kununua uwanja na pikipiki nyingine, baadae akauza 1 akabakiwa na 1 2025 wakagombana na kila mtu akashika njia yake sasa mwanamke anataka wagawane mali yaani kiwanja na pikipiki sasa iyo imekaaje kisheria nisaidieni WANASHERIA.
 
Duh! Ngoja waje wataalam kutoa mwongozo.
Ila wangekaa wasettle tofauti zao.

Kwahiyo mwanamke keshajiandaa kuwa single mother!
 
wanafamilia moja wamekuja kwangu wanataka wagawane mali walizochuma ndipo nikaomba kujua historian yao hadi kufikia hapo, ipo ivi.
Ilikuwa 2018 mahusiano yao yalianza na wakati huo mwanaume alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni moja aliajiriwa, ilipofika 2019 alifukuzwa kaz na kipindi chote icho walikuwa kwenye mahusiano na huyo binti alikuwa mjamzito na anaishi kwao, huyu mwanaume alikuwa na hakiba kidogo bank akachukua hiyo hakiba yake akanunua pkpk ili kuendesha maisha hadi yule mwanamke akajifungua wakat huo mwanaume bado anasubiri peza zake za ppf, 2020 yule binti akajifungua mtoto wa kiume, akaamua kumchukua na kuishi nae lakini hakumuoa wakawa wanaishi tu, pesa za ppf zilipotoka yule mwanaume akaamua kununua uwanja na pkpk nyingine, baadae akauza 1 akabakiwa na 1 2025 wakagombana na kila mtu akashika njia yake sasa mwanamke anataka wagawane mali yaani kiwanja na pkpk sasa iyo imekaaje kisheria nisaidieni WANASHERIA.
where it is proved that a man and woman have lived together for two years or more, in such circumstances as to have acquired the reputation of being husband and wife, there shall be a rebuttable presumption that they were duly married but It is a well settled position that the onus of proving existence or non-existence of any fact lies on the party asserting its existence or non-existence and in civil cases proof is at balance of probabilities meaning the plaintiff must prove that their claims are more likely valid than not.

kiufupi ni kuwa huyo mwanamke aende akafungue shauri mahakamani akathibitishe kuwa kwenye izo mali kuna mchango wake katika upatikanaji wake

Soma kesi ya Sami James vs Pendo Methusela Masalu (PC Civil Appeal 468 of 2023) [2024] TZHC 8615 (10 October 2024)

pia soma S.160 (1 and 2) & S.114 za LMA.
 
Kuna kile kisheria cha kipuuzi kinasema mkiishi kwa zaidi ya miezi sita sijui mwaka kama mke na mume basi mtatambulika kama wanandoa.
 
Chini ya dhana ya ndoa, Huyo mama ana Haki ya kupata mgawo, japo sio 50/50 labda athibitishe alikuwa na mchango unaopimika katika kupata Mali hizo.

Kwenye dhana ya ndoa, hakuna talaka. Ila mahakama itawatenganisha pamoja na kutoa amri ya mgao
 
Back
Top Bottom