Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 414
- 412
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Silas Lucas Isangi akikabidhi vifaa vya Michezo kwa nahodha wa timu Dectaforce Boniface na Msaidizi wake Hamida Nassoro Mussa Kwa niaba ya Wanariadha 9 na Kocha mmoja wanaokwenda kwenye Mbio za Dunia za Nyika Huko Belgrade, Nchini Serbia.
Rais amekabidhi vifaa hivyo Kwa Wanariadha 9 ; Wanawake 4 na wanaume 4 kwa timu ya wakubwa (Seniors)
, na Mwanariadha mmoja wa kiume wa Mbio hizo Kwa kilomita 8 kwa umri wa Chini ya miaka ishirini (U20) "Junior" ambaye ni John Nahhay Wele pamoja Kocha Marcelina Gwandu , katika kambi ya timu hiyo iliyokuwa jijini Arusha, ambapo wanatarajia kwenda kushindana Mbio hizo tarehe 30/03/2024 Huko Serbia.