Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,003
- 20,382
Kwamjibu wa nyaraka za MOSSAD, CIA, RAW na FSB juu ya elimu ihusuyo "kiwango cha hali ya hatari katika eneo la kiraia na kijeshi" ambacho hupimwa kwa kipimo kiitwacho Def Cond, (defence Control) inasema, "Pale majadiliano ya meza yanaposhinwa kuleta jibu chanya, wanamjadala hususia meza, ambapo katika kipimo husomeka Def Cond 0001".
Ikitokea kuwa hata huko walikoamua wanamjadala hao kupeleka hisia zao nako kukazuiwa, hasira ya wanamjadala hao huongezeka na kuwa Def Cond 0002.
Hatua ya mwisho ya wanamjadala hawa huwa ni kwenda kwenye mahakama ya umma, hapa kipimo husomeka Def Cond 0003.
Hiki ni kipimo kikubwa katika medani ya kiusalama kwa mambo ya ndani, ambapo matokeo yake shughuli katika jamii husimama, serikali hushindwa kutawala wala kuongoza. Katika lugha nyingine huitwa mgogoro wa ndani,kisiasa,kikatiba nk...
Zingatia hali hii haizai vita, kwani ili vita kamili ya ndani izaliwe lazima hali ya hatari isomeki Def Cond 0006. Na ili vita kamili izaliwe katika ya taifa na taifa lazima hali ya hatari isomeke Def Cond 0008. Jipe muda wa kusoma Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
Lakini dhana nyingine muhimu ni dhana iitwayo "kuhatarisha usalama wa taifa". Ni neno dogo lakini ni kubwa sana ambapo Tanzania limekuwa likitumika na pengine linatumika vibaya,. Je usalama wa taifa nini? pengine hili ndio swali la msingi zaidi ambalo jibu lake litafungua ukurasa mpya wa mitazamo chanya au hasa. Kimsingi Usalama wa Taifa ni ile hali ya nchi na watu wake kuwa tulivu yenye amani na upendo. Ndio hasaa maana ya Usalama wa Taifa, achilia mbali taasisi/idara ya usalama wa Taifa.
Usalama wa Taifa unaweza kuhatarishwa na mtu/kitu/jambo lolote litakalopelekea nchi na watu wake kukosa utulivu, amani na upendo. Hivi ndivyo inavyoweza kutafsirika pale inapotamkwa kwamba huyu anahatarisha usalama wa taifa. Ni kipimo kipi kinachoweza kutumika kutambua na kutangaza kuwa sasa usalama wa taifa unaharishwa? Jibu ni rahisi tu, rejea kule mwanzo nilikoeleza juu ya vipimo vya hali ya usalama ambavyo kimsingi huamuliwa na baraza la usalama la Taifa.
Mtu yoyote anayehubiri ubaguzi wa kiitikadi/kisiasa, kidini, kikabila, kikanda au kwa namna yoyote ya ugawanyo huyo analihatarisha taifa, na hapa sheria ya usalama wa taifa haijatenga aina za watu hao, awe mchungaji, shehe, Rais, raia au kichaa wote hawa wakifanya hayo watakuwa wanahatarisha usalama wa taifa.
Kwa namna moja pengine ieleweke vipo vikundi vinavyoweza kuhatarisha usalama wa taifa, vikundi hivyo vinaweza kuwa kikundi cha kiserikali kilichopata madaraka kwa nguvu au kwa kuungwa mkono na umma kisha kikageuka kuwa kikundi cha kugawa taifa na kuhatarisha ummoja wa kitaifa uliojengwa katika msingi wa udugu. Vivyo hivyo vipo vyama vya kiharakati, vyama vya siasa, na makindi mengine kadha wa kadha ilimradi yanaleta utengano hayo ni makundi hatarishi.
Na ipo mitazamo kwamba serikali ni chombo sahihi kisichokuwa na doa, sio kweli, serikali ni kikundi kidogo sana tena katika nchi kama Tanzania ni kikundi kisichozidi watu laki mbili, yaani chini ya 1% ya Watanzania ndio hawa huunda serikali. Utendaji wao hauwezi kuwa sahihi kwa asilimia miamoja. Lakini kikundi hichohicho cha serikali kinaweza kuwa ni hatatari kwa usalama wa taifa, kwakuwa kitu chochote kinaweza kuwa hatari kwa taifa, na sheria ya Usalama wa Taifa haijaitenga serikali kwamba yenyewe haiwezi kuwa hatari kwa taifa.
Vivyo hivyo sheria hiyo hiyo haijazuia kwamba Usalama wa taifa haiwezi kuwa hatari kwa taifa. Jibu linabaki nani mwenye ithibati ya kuamua huyu ni hatari kwa usalama wa taifa na yule sio hatari na kwa vipimo gani? Reejeni nchi ya ahadi, sio ccm mpya ya akina Chakuba... Bali Tanzania ya leo na kesho.
Maslahi ya ccm, Chadema, CUF au ACT yakiyumba au kuvunjwa si hatari kwa usalama wa taifa. Mtu kutafuta madaraka ya kichama ama ya kiserikali ndani ya chama, hakuhesabiki kama kuhatarisha usalama wa taifa bali kufanya siasa za medani na tukufu ndani ya chama. Mfano mzuri Zitto na Kitila walipotaka kuondoa uongozi wa Chama hawakuhatarisha usalama wa "Taifa". Wala Lowasa, Membe, nk wanapota kugombea urais 2020 sio kuhatarisha usalama wa taifa.
Mambo hayo yabaki kichama yasifichwe kwenye usalama wa taifa. Chadema iliyashugulikia kichama na chama kikabaki salama, hivyo na ccm iyashughulikie kichama bila kujivika udola,u serikali, kitendo cha wanaozidiwa katika vita ya ndani ya ccm kujaribu kujihami kwa kuyapeleka kiserikali (kuhatarisha usalama wa Taifa) automatic yanageuka kuwa ni mashauri ya uhaini ambayo makao yake ni mahakamani na jela.
Tujifunze mkasa wa Boris Yetsin na shirika la ujasusi la KGB, katika kilele cha ubora wa KGB yenye sifa zilizotukuka ulimwenguni, ilibainika kuwa ni kikundi hatari kwa usalama wa Urusi katika mmeng'enyo wake na GRU hali iliyopelekea mabadiliko ya haraka miaka ya 1994 na kuzaliwa shirika jipya la ujasusi la SFB ambalo sera yake na muundo wake ulibadilika pia na kuzaa Urusi imara ya leo baada ya kuanguka kwa Soviet.
Sisi Watanzania tunaolitakia mema taifa letu, tunawajibu mmoja tu, nao nikuhakikisha kuni haziishi jikoni ili taifa lipone. Hatuna sababu ya kujitazama na kumtazama kila mmoja wetu, tulishabaini wapi tulianguka, ni wakati wa kuinuka, hili litafanikiwa tukilitazama taifa badala ya kutazama vyama, dini, kabila au kanda zetu. Wazalendo wa kweli Malisa, Cyrilo, Levy, Bony Sadru, Hoops, Sambo, Bollen, Thadei na wengine leteni kuni faataaa..!
Nakukumbusha, ziko nakala 10 za Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kwa nusu bei @ 40,000/= tu
Lipia kwa 0715865544 / 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo. Kitabu kitaletwa ulipo.
Na Yericko Nyerere