Mayo clinic
Member
- Sep 1, 2022
- 23
- 22
Yamekuwepo mazoea mabaya sana ya kutowafuatilia wanafunzi wanaoshindwa katika mitihani ya upimaji ya kidato cha pili.Yaani mtoto na mzazi wanaamua wenyewe kama iwe mwisho wa kusoma au arudie darasa.kunakuwa hakuna ulazima tena.
Hali hii imejengeka na kuwa mazoea kiasi kwamba hakuna anaejali.Matokeo Yake ni kwamba kumekuwa na ongezeko la watoto mitaani ambao hawana mwelekeo wowote.
Serikali ni vizuri ikaingilia Kati na kukemea hali hii, kabla haijaota mizizi na watu wote wajue kuwa mtihani wa kidato cha pili,si hitimisho la kuendelea au kutoendelea na shule.