Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 562
- 1,312
Wakuu salam,
Sijui kwa maeneo mengine ila huku mitaa ya Mbezi Beach kwa Zena kuna maboresho ya mfumo ya maji taka ambayo yanafanywa kwa baadhi ya nyumba wanaotaka kuwekewa mfumo huo. Walianza kuweka chemba barabarani na sasa wanaunganisha mifumo hiyo.
Hapa ni kwa mara ya kwanza baada kuweka chemba, hata kushindilia hawakushindilia vizuri, mvua ilipiga, hali ndio ikawa kama mnavyoona hapo (Juni 2024).
Baada ya mvua kupita hali ilikuwa hivi, udongo ukaanza kutitita na chemba zinaanza kuchomoza
Hii ni baada ya kupiga kelele walikuja kushindilia udongo kama inavyoonekana. Kwakuwa ilifanywa kwa kulipulia kwa mara nyingine kadri magari yanavyopita ndivyo udongo unatitia na chemba hizo kuchomoza. Ukiangalia vizuri utaziona kwa mbali. (Julai 2024).
Hii ni Januari 2025, kama mnavyoona chemba zinazidi kuchomoza huku udongo unazidi kutitia, yaani toka Juni 2024 tunaongelea mambo yale yale, inafanyika quick fix ili wapate nafasi ya kuja kupiga hela tena
Sasa wameanza kuwaunganisha watu na mifumo hiyo, tatizo ni kwamba wakija kumuwekea mtu mfumo huo wanafumua njia kisawa sawa, wakishamaliza ndio wanaondoka, hivyo udongo ukiwa umeachwa utafikiri wameandaa shamba kwaajili ya kulima.
Sehemu nyingine ni katikati ya barabara, kutokana na uzembe huu unakuta udongo unakaa sehemu moja kadri magari yanavyopita na kuacha matenki hayo kuchomoza juu ya barabara, hali inayohatarisha usalama wa wapita njia hasa ikiwa unapishana na gari.
Hapa ni baadhi ya maeneo ambayo wanasubiri kuunganishwa na mfumo huo.
Ni hivi ndio inavyoonekana baada ya kuwa wamemaliza kumuunganishia mteja, ka-mvua kalikopita juzi ndio njia imebaki kuwa hivi. Hali iko hivi sehemu zote walikomaliza kuunganisha mifumo hii.
Walau wangekuwa wanamwaga kokoto na kuweka zege ingekuwa afadhali, yaani hapa tunaombea mvua isinyeshe udogo ukauke wenyewe, maana ni kama wametutelekeza. Adha itakuwa kubwa sana hasa kwa watembea kwa miguu na hata wenye magari ya chini kwa sehemu ambazo chemba ziko katikati ya barabara na udongo umetitia.
Dawasa Wizara ya Maji na mamlaka nyingine mnazoshirikiana kwenye mpango huu, niwaambie tu tutawakaba, maana mnafanya makusudi sababu mnaelewa hasara zote zinazotokana na haya mnayofanya lakini bado mnapuuzia.
Maboresho yafanyika, soma hapa ~ DAWASA na TARURA warekebisha barabara zilizoharibiwa kutokana na mifumo ya Majitaka Mitaa ya Mbezi Beach