Wanaoanguka kanisani ni wanaopenda, wapiga picha na mabodigadi hawaanguki kwa sababu hawataki

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
7,164
16,956
Katika kuperuzi huku na kule nimekutana na usahili wa huyu bingwa Kiboko ya Wachawi na mwandishi mmoja.

Anaulizwa mbona mabodigadi, wapiga picha na vinanda hawaanguki kama wale waumini anasema ni kwa sababu hawataki kuanguka, hata waumini wakitaka wanaweza kutoanguka. Ni jambo la hiyari ya mtu.

Kuhusu kutoza watu pesa ya kumuona, anasema imeandikwa aliyenacho ataongezewa, asiye nacho atanyang'anywa hata hicho kidogo. Anasema wanaokwenda kanisani ni masikini, matajiri hawendi kanisani, ndio maana hakuna tajiri aliyefirisiwa nae.

No hayo tu
Siku hizi manabii na mitume wa kiafrika wanakuchana live tu uchague mwenyewe kuwafuata au kutafuta pa kwenda na shida zako
 
Huyu jamaa sijawahi kumuelewa ni msanii sana kajichubua hadi mikono kaziba na gloves
 
Huyu jamaa kuna sehemu nyingine anasema yeye hawezi kuwaambia watu waache dhambi.
Mimi nimevutiwa kumsikiliza, ni mkweli sana katika ulaghai wake.
Anawaambia waumini unaoption moja tu kuingia kanisani na kutabasamu na kusherekea au kutoka ukatafute pa kwenda. Hutaki utafukuzwa.
Ila nilikuwa simjui wiki hii ndio nimemsikiliza kwa mara ya kwanza, siku zote nilikuwa nampuuza. Jamaa anajidai sana, anaona watu ndio wanamtaka yeye sio yeye kuwataka wao. Sanaa yake ya injili anaifanya kwa kurelax sana.
 
Kizazi cha leo kinahitaji udhihirisho wa nguvu za ELOHIMU zilizoandikwa kwenye Neno kudhihirika katika maisha ya watu waliokata tamaa na kukosa tumaini kutokana na changamoto wanazopitia.

Hali hii imechagiza hawa wafanyabiashara ya Injili kuteka fikra na fahamu za watu kwa kujipa umhimu wa kutatua changamoto zao kupitia mafuta, vitambaa, maji n.k.

Kama kanisa kuna sehemu tumekosea au hatukutekeleza wajibu wetu ipasavyo na kupelekea Shetani kusimamisha madhabahu yake kupitia hao wasanii wa Injili.

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako
 
Mkuu mbona sasa hivi ni kama wauongo wanakwenda viral wakati wa ukweli tunafunikwa.

Jes Yesu kashindwa nguvu na Yesu feki?
 
Kuna sehemu hatukusimama katika zamu zetu ipasavyo kusugua magoti mbele za YEHOVA.

Tulilala usingizi adui akapanda magugu shambani mwa BWANA.

Bila neema ya Mungu hawa watu watalitesa kanisa mno maana wamefanikiwa kuteka watu wengi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom